Thursday, September 11, 2008

Peter Tosh. (Oct 9, 1944 - Sep 11, 1987)

Winstorn Hubert McIntosh

Tosh kazini

Wengi wanamfahamu kama Peter Tosh na pia kama Bush Doctor ama Stepping Razor lakini jina lake halisi ni Winston Hubert McIntons. Ni muasisi wa The Wailing Wailers akiwa na Bob Marley na Bunny Wailer., mwasisi wa ile inayoitwa "choppy and syncopated Reggae Guitar Style" na mmoja kati ya wqna-reggae waliokuwa na msimamo mkali na mfumo wa utawala uwakandamizao wanyonge na aliyejijengea maadui wengi kwa tabia yake ya kukemea maovu kwa nyimbo zenye ukali wa maneno ya wazi. Akisimama urefu wa 6'5.5", Tosh anayejulikana kwa kuwa na hasira na mwenye uwezo mdogo wa kukabili hasira zake alijitenga na The Wailers iliyokuwa ikiongozwa na Bob Marley mwaka 1974 na kuwa msanii wa kujitegemea ambapo aliweza kufyatua albamu zaidi ya 8 [ Negril (1975) Legalize It (1976) Equal Rights (1977) Bush Doctor (1978) Mystic Man (1979) Wanted Dread And Alive (1981) Mama Africa (1983) No Nuclear War (1987) I Am That I Am (2001)] kati ya mwaka 1975 - 1987 alipouawa na kundi la watu watatu waliomvamia nyumbani kwake wakiongozwa na "rafiki" yake Dennis "Leppo" Lobban ambaye baadae alijisalimisha polisi na kuhukumiwa kifo, hukumu ambayo ilitenguliwa mwaka 1995 na sasa anatumikia kifungo cha maisha.
Tosh mbali na kuwa askari wa imani ya ki-Rasta, pia alikuwa mpiganaji wa haki za wanyonge hasa wa-Afrika ambapo aliimba mengi juu ya Afrika na Uafrika katika nyimbo kama Mama Africa na African.
Ni miaka 21 tangu Peter Tosh auawe, lakini baadhi ya kazi, imani na maono yake vinaendelea kuwa chachu ya mabadiliko kuelekea mafanikio.
Kujua mengi juu yake bofya http://en.wikipedia.org/wiki/Peter_Tosh

No comments: