Saturday, September 13, 2008

Poleni wana-Houston

Uharibifu uliofanywa na kimbunga Ike.

Kituo cha mafuta kilichoathiriwa na Upepo na maji
Picha toka Reuters na AFP

Kimbunga cha Ike kimefanya madhara makubwa katika sehemu kilizopita na moja kati ya sehemu zilizoathiriwa na kimbunga hicho ni mji wa Houston Texas. Moja kati ya miji mikubwa hapa nchini na ni kati ya mji wenye waTanzania wengi pia waishio na kuendeleza pilika za maisha na mustakabali wa maisha yao.
Tunaomba na kuamini kuwa wako salama, japo twatambua kwa walio waliokuwa katika "njia ya kimbunga hicho" watakuwa wamepata uharibifu mkubwa wa mali zao.
Poleni sana na kila la kheri katika kurejea maisha yenu ya awali.

No comments: