Saturday, September 13, 2008

JUNGU KUU

TAJI "Master T" Liundi
Nikiwa na Master T nje ya studio za zamani za Times Fm (2002)
Katika maisha kuna watu tunaokutana nao ambao kwa namna moja ama nyingine wanakuwa na nafasi ama ushawishi wa kuyabadili maisha yetu. Wanakuwa na upande ambao unaweza kuongoza mengi maishani. Hawa ni wengi na katika nafasi ama fani fulani fulani wanazotuongoza kuelekea kwenye mafanikio wanatambulika zaidi kama MENTORS. Taji "Master T' Liundi bado atabaki kuwa mmoja kati yao maishani mwangu. Kuwa naye ndani ya Studio za 100.5 Times Fm ni kati ya vitu vilivyonisaidia saaana kikazi na sina budi kumshukuru.
Kwa wanaomtambua vema Master T (tangu enzi za asili ya Bongo Flava) wanatambua uwezo wake nyuma ya microphone katika uchambuzi wa mambo mbalimbali, watakubaliana nami kuwa Taji ni "mmoja wa wachache" waliozaliwa kufanya wafanyacho.
Blessings Master T

No comments: