Wednesday, December 24, 2008

Kwa tulio nje ya Tanzania.

Kuna changamoto nyingi tunakutana nazo tunapomaliza na kupanga mwaka MPYA. Na ni vema pia kukumbushana mipango ambayo kama tutaianza pindi tuanzapo "mwaka mpya" basi kuna uwezekano wa kuifanikisha. Kwa wale walio nje ya nyumbani tukumbuke kuwa tuko ugenini na huko hakutakuwa kama nyumbani. Tujue kuwa kama kunapendeza ni kwa kuwa walitangulia walikwenda sehemu kama Afrika na kukomba walichohitaji na kujenga kwao, nasi ni wakati (si wa kulipiza) bali kutumia nafasi kama waliyotumia wao kujenga kwetu. Si unajua huwezi kuishi sokoni, na pia huwezi kuifanya nyumba yako soko? Uliko ndiko ukusanyapo yale ya "kulia kivulini"
Niwaache na Justine Kalikawe ambaye anatukumbusha tulio mbali na nyumbani kuwa tuliko ni ugenini na kamwe sio kama nyumbani. Tafuta utafutacho urejee kujenga na kusaidia nyumbani.
Blessings

1 comment:

Christian Bwaya said...

Kaka Uwe na Mwisho mwema wa mwaka. Ujio wako kwenye blogu umeleta changamoto. Kazi zako zinafikirisha. Nimepedna falsafa yako: Tatizo si tatizo lenyewe, ni vile tunalichukulia.

Nakutakia kasi zaidi mwaka unaoanza siku chache zijazo. Tuombe uzima.