Monday, December 22, 2008

Nyakati hizi nyumbani

Sangara
Vielekezi vya kunyumba. Safi sana
Hapa ndo penyewe. Senene
Ufugaji nao
Sijui yapi ni maembe sindano? Ila matamu
Ukulima nao
Na haya ya kuchoma ukiwa ndani ya basi je?

Inapofika tarehe kama hizi unajua ni wakati wa likizo nyumbani. Ama wewe ama ndugu watarejea nyumbani na kisha nyumba, mtaa, kijiji na kata vyafurika watu. Wakati wa kupeana habari, wakati wa ndugu kukumbukana na kukumbushana mambo ya shule. Kukutana na wale uliosoma nao ambao wanafanya kazi mbali nawe na pia kwa wale tulio mbali kidogo tunapata fursa ya kurejea kwenye vile ambavyo tukiwa huku twavikosa saaaana. Binafsi nawakumbuka wazazi, ndugu jamaa na marafiki. Nayakumbuka mazingira ya kijijini na mfumo mzima wa nguvukazi. Pia misosi yake hasa Matoke na Senene.
Wewe je?

Labda nisindikize hisia hizi na Luciano ambaye anajiuliza ni lini atakwenda tena nyumbani kujumuika na wa-Afrika wenzake kufurahia maisha matamu ya Afrika. Msikilize katika kibao chake hiki When Will I Be Home

10 comments:

Unknown said...

DU! UMENITAMANISHA KWELI.
MSOSI MZURI NA UNAVUTIA, AMA KWELI WATU WA BK WANAFAIDI.

Mzee wa Changamoto said...

Dah Kaluse. Pole kwa kutamani. Lakini naamini sehemu zote wana vyakula vizuri na vyavutia. Basi tu hatuweki kumbukumbu. Ila Kaka Mpangala huwa ananitamanisha saana na dagaa wake na mapochopocho ya Lundunyasa.

Bennet said...

Duh!! haya mambo si mchezo maana kuna ndizi , maembe, mahindi, senene n.k hivi vyakula fresh kabisa toka shamba na utakuta vimelimwa bila mbolea wala madawa na mbegu zake ni za asili

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa changamota tabia mbaya sana kutamanisha watu vyakula kama hivyo. Yaani mate yanandondoka ooohhh hapa nimetamani kweli kweli nyumbani

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kaluse anatamani sennene hii masai vp? teh teh teh! umenikumbusha tulipo kuwa wadogo, msimu wa senene tulikamata, tulisimamisha masomo kwa ajili yao. tulikula kwa furaha, wachumba waliganuzana kama ishara la engagement. tuliwatunzia wenzetu walioko mbali. senene walifungwa kwenye kakamba fualani na kuwekwa juu ya eneo la kupikia ili wasioze wala kuliwa na panya.

hicho kibao cha bukoba, biharamulo na muleba, ukifuata cha muleba, unakutana na kilichoandikwa Izimbya, katerero. basi huwa kinachekesha watuuuu

umenikumbusha kulalila kwa enkoko, engemu pamoja nekicholi. very soon ntakwenda bukoba na kupiga picha nzuri na tamu zaidi

Anonymous said...

Kumbe hawa jamaa wanaitamani Tanzania eee? Nimemsikia huyo kwenye wimbo akijiuliza kama asili yake ni Tanzania. Wimbo bomba saaana huuu. Nimeupenda.

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto una mambo! umenikumbusha nyumbani hasa kwa hiyo picha ya senene na ndizi. harafu hiyo picha ya direction umeipata wapi?kwetu huko nimefurahi sana kuiona! asante sana.

Mzee wa Changamoto said...

Karibu tena Da Sophie. Hiyo picha niliipiga majira kama haya mwaka mmoja uliopita nilipokwenda kuwatembelea wazazi. Nilifurahishwa na mabadiliko kiasi niliyoyaona na naamini yatazidi kuwa bora zaidi nz zaidi hasa kwa manufaa ya wananchi. Kuhusu vyakula kwa hakika nimevikumbuka saana. Unajua ndizi yenye harufu ya "omwika na kashweko" yaani ni tofauti na hizi tufunikiazo ma-nylon huku ili ku-keep steam. Lakini kama wasemavyo kuwa "if you don't have what you like, like what you have" hivyo twalazimika kuweka "psychological tastes" ili kujihisi tuko nyumbani.
Karibu tena na asante kwa kazi nzuri jamvini mwako Dada

Unknown said...

Kaka senene hao duuu!!!
udenda wantoka yani dah, wankumbusha mbali sana na safari sijaenda likizo basi taabu kweli kweli, yaaani hapo namwona bibi Ma Buruke anantengea ktk kiibo na mbwembwe kibao yani dah.

Mzee wa Changamoto said...

We acha tu. Lakini wewe si waweza wekewa kwenye Precionair zikaja? Sie sasa mpaka aje mtu na sio leo ama kesho.
Twala kwa taswira tu Kaka Bernard