Kilelelezo kuonesha uathirika wa Kipindupindu huko Zimbabwe
Joseph Kony Nako UGANDA kumeripotiwa Jumatano ya wiki hii kuwa kikundi ama jeshi la Lord's Resistance Army linaloongozwa na Joseph Kony na ambalo kwa zaidi ya miongo miwili limekuwa likipigana na askari limeua zaidi ya watu 100 katika mji wa Tora ulioko kaskazini mashariki ya Kongo. Hiyo yafanya idadi ya waliouawa na kundi ama jeshi hilo kufikia 900 tangu mwezi uliopita. Ni waafrika wenzetu, wanaotaka kutuletea maendeleo na ambao wanatuua ili kuweza kulazimisha kupatikana ama kutekelezeka kwa mahitaji yao.Bofya hapa kusoma
WOW!!!!
Ndipo nimkumbukapo Winston Rodney a.k.a Burning Spear ambaye katika wimbo wake TOGETHER ameanza kuimba kwa kuuliza swali kuwa "Do you enjoy terrorizing your area? Do you enjoy killing your brothers? Do you enjoy killing your fathers? Africa they use to chain us together." Sijui kuna tofauti gani kati ya mauaji ya "wakoloni" na haya ya sasa maana wote wanaua asilimia kubwa ya wasio na hatia. Burning ameendelea kuwakumbusha waAfrika kuwa twaweza kuwa wamoja, kufanya mambo mema na kuonesha uAfrika halisi alitaja mengi ambayo kama waafrika twaweza kuyafanya kuuonesha ulimwengu yale tuwezayo kuyafanya tofauti na vile walivyotufanya wakoloni. Baadhi ya aliyosema ni pale anaposema "we can show the world that we're not worst kind of brothers, we can show the world that we can live together, we can show the world that we can move together."......."it's getting from bad to worse, throw down your arms and guns"

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:
ndio umesema vyema. ni swali zuri kwamba, kwa nini kuna majamaa yanayofurahia kuuwa wenzao? wewe umeliongelea kibaguzi zaidi kwamba waafrika wenzzao, lakini sote ni binadamu bila kujali makundi.
hawa majamaa wana siri zao na ndio maana hawakamatiki au wankamatika kijinga. ni ile tabia ya binadamu wa leo kupenda mali kuliko utu na ubinadamu wake mbele ya mwingine.
siku zote kuna watu migongoni mwao wanaowapelekea mali wanazoiba na ndio maana huwezi kusikia eneo lisilo na madini, nk linapiganiwa sana.
laikini tatizo ni letu sote. mtu anayetamani anasa, akipewa mkataba mnono kwamba apigane, atakataa? tunahitaji kutanguliza utu na heshima kwa viumbe vya muumbaji vinginevyo tutaishi matajiri harafu tufe masikini
Kuna ukweli katika ulilosema kuwa nimeiongelea kibaguzi zaidi. Labda ni kwa kuwa ninasikitishwa na hali iliyopo ambapo nchi zisizotengeneza silaha na ambazo zimefungiwa kufanya biashara na nchi yeyote barani Afrika ndizo zinazouana tena kwa silaha za kisasa, na ndio wanaoshikilia migodi ya madini kama ulivyosema na nchi zenye kuja na silaha mpya na kali kila mwaka wala hawana haja nazo maana hakuna hata dalili ya vita nchini kwao. Nina makala ijayo iulizayo juu ya hili. Juu ya hawa wapiganaji ambao wana vizuizi vya kibiashara kwa miaka kadhaa na hakuna anayefanya kazi na bado wananunua silaha "made in peaceland". Mkataba ni upi na wanalipa vipi? Na kwanini inapotokea kutoelewana baina yao wanakamatika kiraihisi? Si tuliona Savimbi? Tunaona Nkunda? Sasa ni wangapi wauawe kabla Kony na wengine hawajatiwa mbaroni? Yaonekana wanaweza kukamatika, lakini ni mpaka waoneshe nia ya kuacha "bizinesi" waifanyayo na hao wawapao sapoti.
Asante Kamala na heshima kwako mkuu
Post a Comment