Friday, January 9, 2009

Them, I & Them. LUCKY DUBE........The Other Side

Pengine kama kuna kitu kilichomtofautisha Lucky Dube na wasanii wengine wa Reggae ni namna alivyoweza kusimulia kisa ama hadithi yake yote tangu mwanzo mpaka mwisho katika wimbo mmoja ambao ukimaliza kuusikiliza utaweza kujua hasa alikuwa akizungumzia nini. Lakini pia lugha aliyotumia na kuhusisha nyimbo na mtukio ya wengi (hasa Afrika) vilimuweka katika ramani nyingine.
Hakuna tofauti hapa anapowazungumzia watu wawili wa "dunia" mbili tofauti wanaotamani upande wa pili bila kujua ukweli halisi wa maisha yake. Anamzungumzia Jackson aishiye Jamaica ambaye kila kukicha anakwenda kuitazama bahari anayoamini inamuunganisha na ina majibu ya "kwao" Afrika huku akitamani kwenda huko, na pia anamzungumzia mwingine aliye Afrika Kusini ambaye kila kukicha anaenda uwanja wa ndege kuona zirukavyo akiamini kuna siku ataikimbia Afrika kwenda ambako walioko huko wanatamani kuja aliko. Lucky Dube anasema "i lived his world and i've seen the other world, i've got nothing to say. I put my coat on my shoulder as i walk away i heard myself sing the grass is greener on the other side, till you get there, you see for yourself".
Ndio ukweli uliopo katika maisha ya sasa ambapo baadhi ya walio nyumbani wanatamani ughaibuni na baadhi ya walio ughaibuni nao wanatamani kurejea na maisha ya nyumbani. Kila mtu anaamini kuna "nyasi za kijani' upande wa pili.
Sijui waujuaukweli wa "upande wa pili" kwa kiasi gani kujua maisha halisi waishio kule na nini hasa wahitaji kufanya kabla hujafika na kuanza maisha mapya huko?
Sina la ziada. Msikilize Lucky Dube katika wimbo wake "The Other Side" uliobeba jina la albamu The Other Side iliyotoka mwaka 2003. Ilikuwa ni albamu ya pili toka mwisho kabla hajauawa.
Bofya Player hapa chini kisha fuatisha maneno chini yake kuona / kuelewa ukweli na undani wa alichokisema.

His name is Jackson, he lives in Jamaica
Every mornin' he comes down to the docks
To watch the ships come and go
He's been here too long
Mental slavery, has not touched him one bit

He still know his history, he knows where he come from
That is why he believes the ocean
Can give him some answers
About the very very far home
That he's never been to all his life

He says, "I wish I was home, I wish I was in Africa"
Hey, I wish I was home, I wish I was in Africa

I have seen his world, I've seen the other world
I have nothing to say
I put my coat on my shoulders
As I walk away, I heard myself sing

The grass is greener on the other side
Till you get there and see it for yourself
The grass is greener on the other side
Till you get there and see it for yourself
The grass is greener on the other side
Till you get there and see it for yourself

His name is Themba, he lives in Soweto
Every mornin' he goes to the airport
To watch the planes come and go
He has changed his African name to a western one
'Cause he doesn't know how it hurts
To have a name you can't be proud of

He hopes that one day
One of these birds of the sky
Can take him away to a very very far land
Running away from the very roots
That so many black people in the world
Are wanting to come back to a place they call home

They wish they were home, they wish they were in Africa
They wish they were home, they wish they were in Africa

I live in his world, I've seen the other world
I got nothing to say I put my coat on my shoulders
As I walked away I heard myself sing

The grass is greener on the other side
Till you get there and see it for yourself
The grass is greener on the other side
Till you get there and see it for yourself
The grass is greener on the other side
Till you get there and see it for yourself
The grass is greener


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

tatizo laweza kuwa ni kuishi maisha yasiyoyetu na kuishi kwa majuto na hofu.

kuishi kwa majuto maanake ni kuishi jana na kuishi kwa hofu ni kuishi kesho.

walioko ugaibuni wanajutia kwenda huko jap ohawako tayari kurudi na walioko home wanatamani kwenda majuu wakidhani kuwa huku maisha ni noma. hata mimi natamani kwenda bushi kwetu

Mzee wa Changamoto said...

Na Kamala unajua kama nijuavyo Mimi kuwa walio Bush kwetu wanatamani saana kuionja Darisalama. Sijui kwanini. Lakini uliyosema ni zaidi ya ukweli. Asante Kaka

Koero Mkundi said...

Kaka nimepita kujifunza humu kibarazani kwako,

Ahsante kwa kutukumbusha habari za huyu mwanfalsafa wa Reggae, namfagilia sana.

nimejitahidi kutafuta MP3 ya nyimbo zake lakini hazipatikani hapa jijini DAR.

Mwenye kujua zinakopatikani anijulishe kupitia humu.

Subi Nukta said...

Ndiyo hulka ya mwanadamu na binadamu huridhika kwa njia tofauti. Sehemu moja kwako inaweza kuwa mbaya sana na sehemu hiyo hiyo kwa mwingine ikawa ya manufaa tena ya kukumbukwa sana. Binadamu ndivyo tulivyo!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

lakni bibi yangu alikataa kata kata kupelekwa state wala dar wala mwanza. nadhani ni jiniasi fulani hivi. yuko bush anapunga upepo