Friday, February 13, 2009

Them, I & Them. BERES HAMMOND.....They Gonna Talk

Kesho ni siku ambayo kuna washerehekeao na kuiita siku ya wapendanao. Japo sina imani wala amani na siku hii na japo huwa siisherehekei kwa kuwa mimi na wangu twaziona kila siku kama siku zetu za kupendana, ni lazima kuyaangalia ama kuyajadili matatizo makuu yaikumbayo jamii ya wapendanao. Na hakuna asiyejua kuwa MANENO + MASENGENYO ni kati na vitu vikubwa viikumbavyo jamii ya wapendanao.
Ukweli wa mambo ni kuwa mengi yatasemwa, mengi yatawekwa mbele yako kuhusu umpendaye na hatua ya mwisho ama mwenye kuamua nini cha kuchukua vipi ili iwe vipi ni mmoja kati ya wawili wapendanao. Ni hapa ambapo mambo hukanganyika na kuchanganyika katika familia.
Well!!!!! Naungana na ulimwengu wa wapendanao siku ya leo kuwapa nguzo nyingine ya MAPENZI kuwa KIKUBWA NI KUAMINI NA KUTAMBUA KILE MUAMINICHO NA KUTOONGOZWA NA YALE YASEMWAYO maana kama alivyosema Beres Hammond kuwa THEY GONNA TALK lakini kitakachowabakiza katika mahusiano ni imani na kujuana kwa wawili wapendanao.
Sikiliza wimbo huu huku ukifuatilia maneno yake.
Blessings
VERSE 1
Some things were meant to be
So why not let it be
And stop worrying about it
Long as we know what's in our hearts
We know our inner thoughts, hey
No reason for concern

CHORUS
They gonna talk, they gonna talk, they gonna talk
They gonna say a lot of things about us
You said you know that love is not a sin
But you worry what the people say
When they see me with you
Wonder what the crowd would say
When they find us together
Wonder what the people say
When they know we are in love
Worry what the crowd would say

You pass them on the street yes
Greet you with a smile, hey
As broad as a nile, hoy
They will say all kind of goody goody to you yes
That lingers for a while
All there in your mind
You wanna go you wanna stay
It seems that you can never ever
make up your mind about it, well
But if you know that love is deep within
Why should you worry what the folks will say

When they see me with you
Worry what the crowd would say
When they find us together
Wonder what the people say
When they know we're in love
Wonder what the people say, oh yeah

Wonder what the people say
When they see me with you
And you wonder what the crowd would say
When they find us together
Worry what the people say
When they know we are in love
And you wonder what the people would say, yeah yeah

CHORUS

IJUMAA NJEMA
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

dunia hii bwana, eti kuna siku ya wapendanao yaani!! hii inazidi kuonyesha ni jinsi gani kizazi hiki kimeenda mbali na kanuni za maumbile (amri / maelekezo ya mungu) kwa sababu amri kubwa sana ya maumbile ni LOVE AND RESPECT TO EVERY GOD'S CREATION. sasa majamaa yan siku moja tu ya kupenda kwa mwaka. yashindwe

Mzee wa Changamoto said...

Ndio hivyo Kamala. Ndio siku ya kumnunulia mpenzio kile apendacho, siku ya kumpeleka akale mlo wa gharama, siku ya kumwambia wampenda pengine kuliko mara zote zilizosalia katika mwaka, siku ya kupanga naye mipango ya mapenzi, ni siku ya, siku ya, siku ya.........
Kwa hesabu za haraka haraka mapenzi ni 1/365 katika maisha ya mwanadamu maana ni siku moja kwa mwaka
Simo.