Friday, May 22, 2009

Them, I & Them...LUCIANO.......Cry For Justice

Uchaguzi wa Tanzania unakaribia na ni uchaguzi ambao unaitwa wa ki-DEMOKRASIA. Hiyo tafsiri ya Demokrasia si ya muhimu kwangu maana ilikuwepo hata kabla sijazaliwa na kibaya zaidi ni kuwa jinsi hiyo demokrasia "inavyozidi kukua" ndivyo tunavyozidi kuona wananchi wanavyozidi kuteseka.
Kwa namna fulani hii hunifanya niamini kuwa demokrasia ni kwa watu "wenye nguvu" japo ni sisi tuwapao nguvu hizo za kutunyonya.
Sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi, ni vipi tunaweza kuwapata wataotafsiri demokrasia kwa manufaa ya wananchi? Viongozi wetu (napenda kuwaita watawala na sio viongozi) wa sasa wanatafsirishwa demokrasia na mataifa makubwa. Wanaambiwa "kumuua raia wa nchi yako ni kwenda kinyume na demokrasia" kwa hiyo wanachofanya ni kuingia nchini mwao, kuua raia wao na pengine viongozi wao kisha kuiita hiyo Demokrasia na bado watu wanakaa kimya. Wanachaguliwa rafiki na adui nawanakubali.
Athari za kusikiliza na kufanya mengi ya waambiwayo ni kuyafanya "mataifa" haya kujifanyia watakayo, wakati watakao, kwa yeyote watakaye na vyovyote watakavyo na kisha kutafsiri madhara ya watendayo kwa namna watakavyo.
Tumeona mengi kwa sasa na kwa kuwa hakuna mwenye uwezo wa kusimama na kuwaeleza kuwa wanakosea na kuwazuia kufanya jingine, tujiulize ni kipi wanachofikiria kufanya punde?
Leo tunaye Luciano ambaye katika wimbo wake wa Cry For Justice ameanza kwa kuuliza kuwa "what will they think of next?"
Msikilize na kumsoma hapo chini katika kibao chake kipatikanacho ndani ya albamu yake aliyoiita Jah Words

Intro: What will they think of next?
Tell me what will they think of next?
Verse 1: What an audacity they spreading their Democracy,
Killing Innocent people every day and night
Its hypocrisy they commit atrocity,
Violating our human rights.
They try to control our minds, treating us like swine
They telling us who to love and hate
As if they are so great
Chorus: And no one seem to have the conscience
To tell them they’re wrong.
They go around the world killing people,
Just because they’re strong
Jah sitteth in the congregations
Listening to the poop people’s cry,
They say woo, woo, woo, Jah, Jah, woo
Woo, woo, woo, Mama, woo

Verse 2: Hear them crying! Crying out for justice. Crying out Crying
It’s a fallacy, they spreading their ideology
Captivating the people all over the world.
Because of jealousy they rob our heredity
Still pushing us deeper into poverty
They try to control our minds, treating us like swine
They telling us who to love and hate
As if they are so great

Chorus: And no one has the gut to tell them
That they are wrong.
They go around the world killing people,
Just because they’re strong
Jah sitteth in the congregations
Listening to the poop people’s cry,
They say woo, woo, woo, Jah, Jah, woo
Woo, woo, woo, Mama, woo


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

ijumaa njema nawe Mzee wa Changamoto. Ama kweli unaleta changamoto kwelikweli

Mija Shija Sayi said...

Asante sana Mzee wa Changamoto!!!