Monday, May 25, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa...BUSU PANDE TATU

Dada Yasinta ameuliza swali la KWANINI WATU WANAOANA? (Bofya hapa kuisoma) na katika maelezo yake ameeleza kinachoweza kutafsiriwa kama "kuchuja kwa penzi". Si jambo geni katika jamii yetu. Tumeshuhudia haya yakitokea na kibaya zaidi ni kuwa yanatokea kwa kasi sawa na "uelimishaji" wa mapenzi na upendo baina ya wanandoa.
Ni kweli kuwa kuna haja ya kujua kwa undani na vema nia ya muoaji na muolewaji kabla ya kujifunga "fungo la maisha" ambalo kutoka inakuwa vigumu hasa kama umeshaanzisha uhusiano mwingine wa kuwa na watoto.
Basi siku ya leo katika Zilipendwa tujikumbushe kile kilichoonwa na wana Magnet Tingisha BIMA LEE ORCHESTRA walipoimba juu ya kuchuja kwa mapenzi na ambayo yalitoka kwenye BUSU PANDE TATU za uso na kuelekea ambako kulimfanya muimbaji ajiulize nia ya mumewe.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Mubelwa! asante sana kwa kuendeleza mada hii. Ni kipande hiki cha mziki umeniacha hoi kabisa.