Tuesday, June 2, 2009

Ujinga 360 degrees

Ni kama hadithi ya Kuku na Yai.

"Nothing is so good for an ignorant man as silence; and if he was sensible of this he would not be ignorant."
Saadi (1184 - 1291)

Ukisoma hapa unaelewa nini? Mimi naelewa kuwa kuna uwezekano wa ujinga kumtoka mjinga kabla haujadhihirika mbele ya wengine. Na kama hili lina ukweli, basi kuna uwezekano wa ujinga kujidhihirisha mbele ya wajinga bila mjinga kujitambua
Haya sasa unakaribia msimu wa wale wachache kuwadanganya walio wengi na kujitahidi kutaka kuwaaminisha kuwa ni wao pekee wenye uwezo wa kuwaondolea matatizo waliyonayo na kuwaletea maendeleao lukuki ndani ya miaka mitano ijayo. Wanawafanya hawa wengi wajipuuze, wasijithamini, wasijishughulishe na kutoitambua nguvu ya maendeleo iliyo ndani mwao na kuamini UJINGA kuwa mwanasiasa mmoja ndiye suluhisho la matatizo yao yote waliyokuwa nayo kwa miaka zaidi ay 40 ya uhuru na kibaya zaidi ni kuwa wanaamini kuwa mwanasiasa huyohuyo anaweza kuyatatua hayo ndani ya miaka mitano ijayo. NI UJINGA KUAMINISHWA HIVYO.
Labda hawajaisoma nukuu iliyoko kwenye blog ya Kaka Matondo isemayo "Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni!" Mwl. J. K. Nyerere (April 13, 1922 - October 14, 1999)
Hapa panatufanya tujiulize kuwa mjinga ni nai kati ya wanasiasa na wananchi? "Tumewalima" wanasiasa kwa mengi mabaya watendayo hasa wanapoahidi vile wajuavyo kuwa hawataweza kutekeleza, lakini pia kuna UJINGA mwingine wa wananchi kuamini kuwa kila kitu kinaweza kukarabatiwa na kutengenezwa na wanasiasa.
Kama ilivyo ngumu kutambua ni kipi cha kuboresha kati ya Kuku na Yai ili kupata zao bora, ndivyo ilivyo kwa siasa za Tanzania ambapo tunashindwa kutambua kuwa ni nani mwenye kubeba lawama kati ya Mwanasiasa anayedanganya na kupata kura na kisha kurejea bila kutekeleza lolote aliloahidi na kuahidi mengine na kuchaguliwa tena, ama ni mwananchi ambaye ananunuliwa siku za kampeni na kisha kuwa maskini kwa miaka mitano na ikija "neema" nyingine ya mpito kampeni zijazo ananunulika tena?
Ni kama mduara uliojaa ujinga ndani ya nyuzi zake 360 zinazojumuisha siasa baina ya waongozaji na waongozwaji.
Tunastahili kutafuta suluhisho la haraka kabla "ujinga" mwingine haujapandikizwa kwa "wajinga" wengine kuhitimisha nyuzi za mzunguko kwani katika nchi yetu, tunaona namna siasa zinavyogeuzwa UJINGA 360 DEGREES na hatuonekani kujua pa kuanzia kutibu ujinga huo kwani NI KAMA HADITHI YA KUKU NA YAI.
Desemba 9, Kaka Kaluse aliwahi kuomba wimbo huu wa POLITICAL GAME ulioimbwa naye Hayati Lucky Dube, na kwa kuwa unaendana na "toleo" la leo (na kwa kuwa nimemkumbuka mtambuzi mwenzangu pia), naomba kuwakilisha

Tuesday, 09 December, 2008
Shabani Kaluse said...Leo umenikumbusha kibao cha Hayati Lucky Dube cha Political Games.
Hebu someni Mashairi haya hapa chini, muone jinsi mwanamuziki huyu alivyowachambua viongozi wa Afrika.


How do you feel when you lie?
Straight faced while people cry
How do feel when you promise something
That you know you’ll never do
Giving false hope to the people
Giving false hope to the underprivileged

Do you really sleep at night?
When you know you’re living a lie
To you it is just a job
To the people it hurts to the bone

What do you say to the orphans?
If the woman and men you sent to war.
What do you say to the widows?
Of the men you sent to war
Telling them it is good for the country
When you know it’s good for your ego
What a shame.
Do you really sleep at night?
When you know you’re living a lie
You talking tough, you talking sincerely

Giving false hope to the infected
Giving false hope to the affected.
To you it is just a job
To the people it hurts to the bone.


Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

No comments: