Saturday, September 5, 2009

Tunapenda kushinda, lakini ushindi wa hivi.!!!!

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 60 Elaine Fulps alijishindia zawadi kubwa zaidi katika bahati nasibu iliyoendeshwa na timu ya ligi ndogo ya mchezo wa Basebal huko Texas/ Lakini zawadi yenyeweeeeeeeeeee......ATALIPIWA DOLA 10,000 KATIKA GHARAMA ZA MAZISHI YAKE.
Uzuri ni kuwa zawadi haiishi muda wake ikiwa na maana itakuwepo mpaka atakapofariki. Wengine wanajiuliza kuwa wakati anaingia katika kinyang'anyiro hiki kilichodhaminiwa na Kampuni inayjishughulisha na mambo ya mazishi ALIWAZA NINI? Lakini swali la pili ni kuwa asingeingia angebadili nini? Gharama za mazishi ziko palepale uwe na mdhamini ama la, na pengine ameongeza siku za kuishi kwa kuwa na amani rohoni akijua kuwa akifa hataacha mzigo kwa familia yake.
Kwani wewe unadhani ungeona tangazo la shindano hilo ungefanyaje? Ungekubali ama ungeogopa kushiriki? Jiulize, walioshiriki WALIWAZA NINI?
Habari kamili juu ya tukio hili iko HAPA

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaziiiii kwelikweli:-)

EDWIN NDAKI (EDO) said...

hii ndio dunia ukishangaa ya musa utayona ya Firauni

Faith S Hilary said...

Ajiue basi..lol.. but its not fair maana zawadi yenyewe hata hufaidi...well i don't know that kwasababu I am not dead...

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Ndugu yangu nimepita kukujulia hali lakini naona bado nawewe unaogopa kushinda zawadi ya kublog ambayo zawadi yake ni kushinda online 24hrs..aa aa

tutafika tu

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duh, italipa mshahala wamzikao