Saturday, September 5, 2009

Vipengele vipya

Katika kuendelea kujuvyana hili na lile na kuviweka katika utaratibu wa kuweza kurejereka kirahisi. Nimeamua kuongeza labes / vipengele viwili vipya. Cha kwanza ambacho kitaitwa MWANANCHI MIMI (Wazo toka kwenye blogu ya Kaka Fadhy Mtanga) kitakuwa kikionesha, kuthaminisha na kuendeleza juhudi mbalimbali zinazofanywa na wananchi wenzetu / sisi wananchi katika kuisaidia jamii yetu. Hapa ni mahala ambapo hata wewe msomaji unaweza kuungana nasi kuonesha unathamini kazi ya mtu fulani kwa jamii yetu. Utakapotuma post kuhusu hilo, itawekwa hapa bloguni katika label hiyo ya MWANANCHI MIMI kuonesha tunavyothamini juhudi za ziada zifanywazo na wenzetu katika kuiboresha jamii yetu. Wapo wengi saana lakini hawapati thamani ya kazi zao kama ambavyo ingestahili na pengine ni kwa kuwa hawako katika "channel" ya kuvutia vyombo vyetu vya habari.
Na kipengele cha pili ni cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya UJINGA na kujikuta wakiingia matatani. Wale watendao ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Na swali hilo ndio litakuwa jina la kipengele cha pili. Yaani kitaitwa WALIWAZA NINI? na kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote.

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Mkuu, awali ya yote nakushukuru sana kwa kunithamini MWANANCHI MIMI. Pia nakupongeza sana kwa kuwa mbunifu zaidi. Twasubiri kwa hamu, haya ndiyo mafanikio ya mwaka wako mwingine katika kublog.
Ubarikiwe zaidi.

Yasinta Ngonyani said...

Nami nasema nasubiri kwa hamu sana maana inaonekana ni mambo mapya kwelikweli na hamu ndo inazidi kuwa.