Wednesday, November 25, 2009

Labda "akutendeaye mabaya" ndiye akujaliye!!!!

Mara kadhaa katika blogu zetu za kimaandishi tumejadili kuhusu suala la UBAYA. Kuanzia kuuangalia kama upo mpaka kuona kama kile kiitwacho ubaya kama kina faida na kisha kuangalia kama tunahusisha lile liitwalo UBAYA na matukio halisi ya maisha yetu. Tumejadili pia kuhusu KUWAOMBEA WALE TUWAONAO KAMA ADUI ZETU kwa kuwa nao wana nafasi kuuubwa saana katika ukuaji wetu. Yaani wanapojitahidi kuhakikisha tunashindwa, wanatuongezea moyo na maarifa ya kufanya vema zaidi. Watu hawa pia ni muhimu saana kwetu. Lakini pengine la kujiuliza ni kuwa LIPI TUONALO KAMA UBAYA?? Unadhani tafsiri yako ya UBAYA inaweza kuwa na ukweli katika kuleta suluhisho la nani kakufanyia nini? Waswahili wanasema TENDA WEMA NENDA ZAKO, nami najiuliza kama ukitenda wema (ilhali atendewaye auona kama ubaya) kisha ukaenda zako unadhani mtendewa atagundua kuwa ni wema kama halitatokea baya zaidi ya ulilomtendea??
Ninavyozidi kuishi nazidi kugundua kuwa pengine akuibiaye sasa hivi shilingi laki moja anakukumbusha na kukuonya kuwa mahala hapo si salama na usiwe unabeba pesa hovyo kabla hujajenga tabia hiyo na kuanza kutembea na milioni kisha zikaibiwa.
Labda mkioana na kuachana ndani ya miezi michache si mkosi bali yaweza kuwa nafuu kuliko kusubiri baada ya miaka kumi ya kuchuma pamoja na watoto kadhaa kisha mmoja wenu analazimika kubaki kwa ajili ya "matunda" hayo mlovuna pamoja.
NI WAKATI AMBAO TUNATAKIWA KUTUMIA KILA KITUKUTACHO KUJIFUNZA NA SI KULAUMU NA KULALAMA
Labda nikukumbushe "hadithi" hii inayoweza kuoanisha vema nisemayo na "kichwa cha habari"

IF YOU ARE UNHAPPY.
Once upon a time, there was a noncomforming sparrow who decided not to fly south for the winter. However, soon the weather turned so cold that he reluctantly started to fly south. In a short tile ice began to form on his wings and he fell to earth in a barnyard, almost frozen. A cow passed by and crapped on a little sparrow. The sparrow thought it was the end. But, the manure warmed him and defrosted his wings. Warm and happy, able to breathe, he started to sing. Just then a large cat came by and hearing the chirping, investigated the sounds.
The cat cleared away the manure, found the chirping bird and promptly ate him.

THE MORAL OF THE STORY
1: Everyone who shits on you is not necessarily your enemy.
2: Everyone who gets you out of the shit is not necessarily your friend.
And
3: If you're warm and happy in a pile of shit, keep your mouth shut.

11 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka Mubelwa, ubaya ukiutazama vizuri wakati fulani una umuhimu. Mtu anapokufanyia ubaya anakupa changamoto ili ukazane katika maisha. Kuna mwanamuziki mmoja wa dini aliimba kuwa mwombee adui yako aishi miaka mingi ili ayaone mafanikio yako. Nasi hutokea tukawatendea ubaya watu wengine. Lakini si jambo la kiungwana kabisa.

nyahbingi worrior. said...

Baada ya kutengana na mchumba wangu hapa majuzi,tulitukanana sana lakini baadaye nilipojigundua nilikwenda kuomba msamaha ili tuishi kwa amani.

maisha na mapenzi.

Upepo Mwanana said...

Nyahbingi ulifanya la maana sana!

Yasinta Ngonyani said...

Ninmeipenda makala hii na ni kweli mara nyingi tumeongelea haya. Kwa mfano niliongelea kuhusu dada yangu mmoja alivyo mbaya lakini si neno nimemsamehe.Ninanukuu kicha cha habari "Labda akutendeaye mabaya ndiye akujaliaye!!!!" Ni kweli kabisa na pia mtanda hakumbuki ila mtendewa ndiye anayekumbuka. tenda wema usingoje shukrani hapa duniani.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kuna matukio tu! ubaya na uzuri ni kwa tafsiri zenu tu.

tuwe chanya labda kuliko kuwa hasi.

ila unadhani jamaa wanaotengeneza Siraha hasa zile za mbagala ni wazu... no, namaanisha waliozinunua, je kwa nini usiongelee uzuri unaongelea ubaya? sio vibaya kweli?

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kama isemavyo ile kanuni ya ukinzani, mimi nadhani ubaya na wema vinakamilishana. Na kama walivyosema Fadhy na Kamala, pengine ubaya na wema vinatawaliwa na mitazamo yetu tu. Leo hii nikikaa na kufikiria vizuri naona pengine bila kutendewa "ubaya" na watu (tena wengine wa karibu sana) nisingeweza kupata motisha wa kujisukuma mbele na kujibidisha zaidi katika shughuli zangu. Tukiuchukulia "ubaya" kama changamoto yetu basi tutakitazama kila kitu (hata kile ambacho tunadhani ni kibaya) katika mtazamo mpya - mtazamo chanya!

Faith S Hilary said...

...The 6 billion people in this world...all of them are very interesting and all of them can't like everything and everyone...I guess its life and we all face...

Mzee wa Changamoto said...

Nakubaliana na mitazamo yenu Kaka Fadhy, Kamala na hata Kaka Matondo. Nakubaliana nawe Da Yasinta na naungana na Upepo mwanana kumpongeza Nyabhingi Warrior kwa uamuzi wake.
Labda ninukuu nilichoandika kuhusu MTAZAMO wa "ubaya" kuwa
Ninavyozidi kuishi nazidi kugundua kuwa pengine akuibiaye sasa hivi shilingi laki moja anakukumbusha na kukuonya kuwa mahala hapo si salama na usiwe unabeba pesa hovyo kabla hujajenga tabia hiyo na kuanza kutembea na milioni kisha zikaibiwa.
Labda mkioana na kuachana ndani ya miezi michache si mkosi bali yaweza kuwa nafuu kuliko kusubiri baada ya miaka kumi ya kuchuma pamoja na watoto kadhaa kisha mmoja wenu analazimika kubaki kwa ajili ya "matunda" hayo mlovuna pamoja.
NI WAKATI AMBAO TUNATAKIWA KUTUMIA KILA KITUKUTACHO KUJIFUNZA NA SI KULAUMU NA KULALAMA".

Na ndio maana hadithi hiyo inaonesha kuwa ng'ombe aliyemnyea ndege (jambo ambalo pengine lingeonekana kuwa baya) alikuwa na jema zaidi ya paka aliyemtoa ndani ya kinyesi hicho na kumla.
Nadhani ndio lengo kubwa la kuandika hii hadithi kuwa NG'OMBE ALIYEMNYEA NDEGE ALIKUWA NA NIA NJEMA KULIKO PAKA.
Blessings

twenty 4 seven said...

big up kwa changamoto nzuri....

Simon Kitururu said...

Asanteni wote kwa shule hii!

徵信社 said...

I love it! Very creative!That's actually really cool.
謝謝你的文章分享,請你有空到我

參觀,Thanks!:))))