Thursday, November 19, 2009

TUWA-USA.......MASHUJAA WETU

Wasomi, wanaharakati wanaosaidia elimu nyumbani
"Do you see the smiles on their faces
after you have done what you do best.
Do you see satisfaction on their faces
after you have blessed them with your gift.
You don't think it's much
but to them it means the world.
They wake up in the morning and wish you were there
You don't have to lie to gain their trust.
You have never won a Nobel prize,
they have never seen you on the TV
your little contribution makes their lives a little bit better every day
YOU ARE A HERO, YOU ARE A HERO."


Haya maneno ndiyo aliyoanza nayo Phillip Lucky Dube katika wimbo wake HERO alipokuwa akitoa heshima kwa wale ambao wana nafasi ndogo katika jamii lakini wakizitumia ipasavyo kuleta MABADILIKO CHANYA KWA JAMII YAO. Nami leo sina ninaloweza kupunguza ninapowafikiria hawa wanachama wa Chama Cha Wanawake Wasomi wa kiTanzania waliopo nchini Marekani ama The Tanzanian University Women's Association (TUWA-USA)ambao hivi karibuni walifanikisha moja ya adhma zao kuu kwa kuwezesha kupatikana kwa madawati 32 yenye zaidi ya thamani ya shilingi 1,892,000 kwa shule ya msingi Mtakuja ambayo ni moja kati ya shule nyingi sana zenye uhaba wa madawati nchini. Mlezi wa TUWA-USA Meja Jenerali mstaafu Benjamin Msuya akimkabidhi Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Kinondoni Bwn Faustine Kikove moja ya madawati 32 yaliyochangwa.
Madawati hayo yaliyokabidhiwa na mlezi wa Chama hicho Meja Jenerali Mstaafu Benjamin Msuya ni hatua kubwa katika kusaidia kuimarisha mazingira ya elimu nchini hali itakayosaidia kuwafanya wanafunzi kufanya vema darasani. Si kwa wanafunzi tu, bali pia mchango huu uliwezesha ajira kwa mafundi seremala
Kinachonipa faraja zaidi ni namna ambavyo wanachama wa TUWA-USA wameweza kufanikisha hili licha ya MAJUKUMU MENGI waliyonayo kimaisha. Chama hiki kinaendeshwa kwa kujitolea na wanachama wake wana majukumu ya kifamilia zaidi (wengine wakiwa ni kinamama wanaolea familia na wengine wakisafiri kutoka majimbo ya nje ya hapa DC Metro ili kufanikisha nia yao) na wamekuwa wakifanya hata mikutano kwa njia ya simu ili kufanikisha adhma yao. Leo hii kuona wanafanikisha hili katika mazingira magumu kama haya inaongeza furaha na kunikumbusha alichoimba Nasio Fontaine kuwa "harder the battle, yougher the fight, SWEETER THE VICTORY"
Blog hii ilibahatika kushiriki katika matukio ya kusaidia kutunisha mfuko ili kiweza kufanikisha jambo hili (kama ilivyoliripoti HAPA)na ilijionea CHANGAMOTO mbazo kinamama hawa wanakabiliana nazo katika kusonga mbele, na leo NAWIWA furaha kubwa kuleta shukrani kwa wanachama wote kwa kusimama imara katika azma yao na kuifanikisha jambo hili ambalo ni ZAWADI KWA JAMII NZIMA YA KITANZANIA. Mwl Albert Juakali wa Shule ya Msingi Iboma wilayani Chunya mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya m'buyu.
Vyama ni vingi, JUMUIYA ni nyingi na mahitaji ni mengi, na ni sisi wenyewe tunaohitaji kusimama kidete kuweza kufanikisha tatizo hili na kuboresha mazingira na maisha bora kwa kila mwanafunzi kwa kujitolea kile tuwezacho katika kufanikisha azma hii. Si lazima kiwe kikubwa, bali tukitoa kwa moyo kitafaa. Kama alivyosema Mother Theresa kuwa "I can do no great things. Only small ones with GREAT LOVE." Nasi tuungane katika kuchangia na kufanikisha kuwaondoa watoto katika mazingira haya. Kama TUWA-USA wameweza kusimama katika MALENGO yao kama walivyoeleza HAPA, ni kwanini vyama na jumuiya nyingine zisiweze??
Licha ya kusaidia kuinua elimu kwa watoto (hasa mabinti) nchini anzania, TUWA-USA imekuwa ikijitahidi kufanikisha njia za kuwezesha waTanzania walio hapa kujua namna ya kupata elimu bora hapa nchini (BOFYA HAPA)
Unaweza kujua na kujifunza mengi kuhusu TUWA-USA kwa kutembelea tovuti yao HAPA
Kwa Dada zangu wa TUWA-USA.
ASANTENI SAANA.
TWAWATHAMINI, TWAWAPENDA, TWAWAOMBEA NA KUWATAKIA HERI KATIKA KILA JEMA MPANGALO KUFANYA KWENU NA KWA JAMII YETU
Kwa blog ya Changamoto Yetu, ninyi ni
HEROES
BLESSINGS
Picha toka Blogs za Kaka Issa & Ahmad Michuzi

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yep na haya ndiyo mabadiliko tunaypaswa kuyaleta.sasa na sisi jumuiya ya wanablogu waTanzania tuanznishe michango ya kompyutua na inernet na mingineyo kule vijijinikwetu ili tulete mabadiliko

Mzee wa Changamoto said...

Kaka UMENENA. Nimekuwa nikiwaza namna ambavyo tunasherehekea SIKU YA KU-BLOGU ULIMWENGUNI na naamini hii itakuwa njia njema. Kukusanya hiki na kile, hili na lile ili siku ya siku ikifika tuongee na kupanga na wawakilishi kama ninyi mlio huko kujua wapi pa kupeleka msaada huo. Hakuna haja ya sote kuwa mahala pamoja. Hawa watu wa TUWA-USA wana majukumu ni balaa, wanakutana kwa simu (conference calls) na bado wanaweza.
Ni kwanini sisi tushindwe?
Binafsi naweza kuungana nawe kuanza kupanga tunachoweza kufanya mwakani. Na kwa atakayetaka kujiunga (naamini wako wengi) basi na afanye hivyo kwani hili huwa linapendeza likifanywa kwa HIARI na kwa moyo mkunjufu
Kwa mara ya tena, ASANTE kwa changamoto iliyoboresha mawazo yangu
Blessings