Monday, November 16, 2009

Za Kale va Maisha ya Sasa.....OGOPA TAPELI

picha toka www.christophercocca.wordpress.com
Wakati mwingine nashindwa kujua kinachotenganisha matendo ya WIZI, UFISADI, UTAPELI na mengine ya aina hiyo kwani yote huishia kuweka machungu ya kupoteza kilicho haki yako kwa mtu ambaye hakustahili na anayechukua chako / vyako kwa namna isiyostahili. Labda majina hayo ni "fasheni" ili kukata makali ya matendo yao ama ni muhimu katika kuwezesha sheria kuchukua mkondo wake kwa mujibu wa tafsiri yao.
Lakini wote (wezi, mafisadi na hata matapeli) wanaendeleza kilio. Jana nimemsoma Dadangu Dinah akieleza alivyoibiwa pochi yake na adha aliyoipata baada ya kupoteza vitu vingi muhimu vilivyokuwa ndani ya pochi yake. Dadangu Koero naye akaandika walivyopoteza karibu kila kumbukumbu waliyokuwa wametunza kwenye kamera yao wakitoka msibani kwa kuwa tu mtu mwingine ameona kuna aliyechuma na kurundika na sasa ni wakati wake yeye kutwaa (tena bila ruhusa).
Kwa nyakati tofauti tumeshuhudia sehemu nyingine za nchi yetu zikijulikana na kupewa umaarufu wa wizi. Bado viongozi wetu wanaendelea kulitumbulia macho (kwa kuwa tu hawaelekei maeneo hayo hivyo hawaathiriki na wizi ama utapeli ama u-kanyaboya huo).
Lakini haya si ya kushangaa kwani yamekuwepo miaka mingi tu na hakuonekani kuwa na sheria "zitakazotoa fundisho" kwa wale wanaoshiriki katika matendo kama haya.
LABDA NI WAKATI WA KUONYANA, KUKUMBUSHANA NA KUSAIDIANA KUEPUKA KADHIA HII KWANI KWA SISI AMBAO YAMESHATUKUTA TUNATAMBUA MAUMIVU NA KADHIA YAKE. NA KWA WALE AMBAO HAMJAKUTWA, (TRUST ME) HILI LA KUIBIWA AMA KUTAPELIWA NI KATI YA VITU USIVYOSTAHILI VIKUKUTE ILI UAMINI
INAUMA
Tujikumbushe yaliyoimbwa nao Vijana Jazz Band kuhusu hawa MATAPELI katika wimbo OGOPA TAPELI ambao ulipata kuvuma saana miaka hiyo. Hata hivyo ujumbe wake ukingali hai hivi leo.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia siku za Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa mtazamo wangu hii yote inatokana na ukosefu wa kazi. Nina maana hawana kazi za kufanya, kazi zao ni kuzurura, hawana elimu. Hii ndio sababu ya kuwadhurumu wengine kuchukua vya wengine bila ruhusa.

twenty 4 seven said...

big up kaka..