Monday, November 9, 2009

Za Kale vs Maisha ya Sasa....SIRI YAKO

Wengi tunajua kuwa kitu kikishaitwa SIRI basi ni cha kuweka mawazoni na kujitahidi kadri ya uwezo wako kutokisema kwa mwingine. Na kuna faida kubwa sana ya kutotoa siri (hasa kwa asiyehusika). Lakini vipi kuhusu UPANDE WA PILI??? Tumeshatafakari kuhusu FAIDA za mtu kuwa na mahala pa kutoa siri?? Tunaona wale wenzetu waendao KUTUBU kwa viongozi wao wa dini na kusamehewa "mizigo" yao na "kuwa huru" tena baada ya kutua siri hizo. Tunao wale wanaokwenda kwa wataalamu wa afya waliobobea kwenye mambi ya akili na ushauri kueleza siri na matatizo yanayowakumba na hivyo kutua mzigo mkubwa unaosonga akili zao. Lakini vipi kwa wale ambao wanaelezwa siri hizo na HAWARUHUSIWI kuzitoa?? Unadhani wanapokutana na matatizo kama hayo waliyoshauri ama kusikia watafanyaje?? Mfano mzuri ni Alhamis iliyopita ambapo mtaalamu wa ushauri katika jeshi la Marekani alifanya mauaji kwa askari wenzake 13. Kazi kubwa aliyokuwa akiifanya kwa miaka 4 ilikuwa kuwashauri askari warejeao toka vitani, ambao wametingwa na msongo wa mawazo (stress). Kwa askari hao kulikuwa na unafuu baada ya kuongea na "mtaalam" lakini kwa mtaalam alikuwa akizidi kurundika taswira mbalimbali za kutisha kuhusu vita (NILIYAJADILI HAPA). Sasa ilikuwa zamu ya Daktari huyu kwenda vitani kukutana na yote aliyosikia lakini hakuwa na mahala pa "kuyatua". Matokeo yake ni kuvuka mipaka ya ufikiri wa ki-utu na kufanya aliyofanya.
UNADHANI ANGEKUWA NA MAHALA ANAPOPAAMINI NA KUTOA SIRI ZOTE ALIZONAZO ANGEFANYA ALIYOFANYA???
Turejee Jumatatuni na kukutana na wana Bima Lee katika wimbo wao, SIRI YAKO.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**

3 comments: