Saturday, December 12, 2009

Flying Snake

Nikiwa Nachingwea nilisimuliwa kuhusu "asili" ya wilaya hiyo. Walionisimulia walisema kuwa wilaya nzima ilikuwa shamba la karanga enzi za ukoloni na kukawa na tatizo kuuubwa sana la panya kula karanga hizo. Nikasimuliwa kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo (la panya), wakoloni waliagiza nyoka na kuwapandikiza ili kuwasaka panya hao na kuwala chini kwa chini. Matokeo yake ni kuwa baada ya kumalizika kwa ukoloni wamebaki wamejazana huko.
Niliona nyoka wa aina mbalimbali, nikaambiwa kasoro na mapungufu yao mbalimbali, lakini sikuwahi kuona anayeruka kama huyu.

ULISHAWAHI KUMSIKIA HUYU???

13 comments:

Fadhy Mtanga said...

Duh! Duniani kuna mambo. Mi ndo nasikia leo. Ahsante sana kwa ufahamisho huu.

Anonymous said...

Hawa nyoka wa kuruka, nimeshuhudia tangu nikiwa mtoto mdogo kabisaaaa, huyu wa kijani akiruka kwenye miti yetu kwetu huko milimani, bibi aliwahi kuniambia, wa kijani anaruka sumu yake kali lakini si sana na si wachokozi, mweusi anatambaa na sumu yake kali sana na ni walionuna, na wale wa kahawia na umadoa madoa hivi, hao ni wabaya sana kaa mbali mno, kisha akamalizia na wale wanaokuwa juu ya mti na kazi yao kudunga utosi wa watu wanaopita chini. Tangu siku hiyo amesema hivyo, wiki nzima nikawa natembea mikoni kichwani kuzuia nisidungwe na nyoka (akili yangu haikunituma kuwa hata mkoni ukiwa juu ya kichwa akiamua kukudunga hajali mkono - ndiyo utoto tena).
Yaaa, nyoka wa kijani huruka I knew it tangu nikiwa chuchu chuu.

Mzee wa Changamoto said...

Hahahaaa Subi.
Umenikumbusha mbaali sana. Nikiwa Nachingwea (nilikuwa mtoto wakati huo) wala sikuogopa nyoka. Tuliambiwa kuhusu UDHAIFU wa kila aina ya nyoka maarufu. Kulikuwa na nyoka aliyekuwa akikimbia saana mti hadi mti lakini hakuwa na sumu hata kidogo. Kulikuwa na kifutu ambaye hasogei (literally) lakini akikuuma ile mpaka ukasikia ka-mluzi, ujue wewe wa kukata mguu. Kulikuwa na aina nyingi za nyoka mpaka kuna mmoja niliyemuona nikashindwa kumuua (japo huwa siwakawizi). Alikuwa na rangi nzuri nikaishia kumkodolea macho akichikichia.
Tukafundishwa kuhusu HARUFU za nyoka kama CHATU na wengine. Pia kuhusu Simba ambao walikuwa wakivamia saana kule. Tukafunzwa udhaifu wao, kulikuwa na chui pia nao tukaelezwa kuhusu wao. Mwisho likaja la huyo nyoka anayedunga kichwani. Siku moja tukasimuliwa walivyokuwa wanaenda kumuua. Sikuweza kushuhudia ila nyoka yule ana sumu saana lakini inamchukua muda kuikusanya. Hivyo wanapika uji wa njegere (kama sikosei) kisha wanamtwisha mtu kichwani akiwa na chungu. Then wanakijiji wanamfuata nyuma wakiimba. Nyoka atajua muda umefika kisha anaanza kujiandaa kumdunga yule "shujaa". Baada ya kufika pale, anajikuta akitumbukiza kichwa kwenye uji na yule "shujaa" anaangusha chungu na kukimbia. KAZI KWISHA
Kulikuwa na nyoka mmoja anakaa juu sana ya mti na alikuwa na mti wake (aina moja tu) anaokaa. Wananchi wakachanga na kununua viwembe na kuvishindilia kwenye gome. Kisha wakaenda kumuwashia moto wa pilipili (unaowakimbiza nyoka) akatoka mbio mpaka mtini kwake na wakati akipanda akajikata. Nyoka hawaishi na majeraha. Akafa baadae.
Kuna njia nyingi wanazotumia wananchi kuwatambua, kujikinga na hata kuwaua hawa.
Labda siku nyingine ntakusimulia nilivyoshuhudia wakimsaka na kumuua Simba mla watu.
Hiyo itaendelea TOLEO LIJALO
Hahahahaaaaaaaaaaaaaa

NASUBIRI MAONI YA MTAALAMU WA HAYA Kaka BENETT

Albert Kissima said...

Hivi ni kweli kuwa chatu akimviringishia mtu kwa ajili ya kummeza, akichapwa na kafimbo chembamba tu husikia maumivu makali kiasi cha kukimbia?

Naomba kuwasilisha swali za ziada.

Albert Kissima said...

Hivi ni kweli kuwa chatu akimviringishia mtu kwa ajili ya kummeza, akichapwa na kafimbo chembamba tu husikia maumivu makali kiasi cha kukimbia?

Naomba kuwasilisha swali za ziada.

Faith S Hilary said...

I wish I could watch this video maana it sounds very interesting lakini I am terried of snakes...kama haitishi sana kwa watu wenye hii phobia...please let me know blog author

Mija Shija Sayi said...

Hii imenikumbusha nikiwa shule ya msingi Nyamagana Mwanza, tulikuwa tukicheza mpira wa rede chini ya mti basi aliruka nyoka toka juu ya mti na kutukosakosa, na mpira ukaishia palepale inasemekana alikuwa ni wale wa kudunga utosi.

** da Subi umenifurahisha na staili yako ya kutembea mikono kichwani kweli utoto kazi.

Mzee wa Changamoto said...

Kissima, sina hakika na hili, lakini awa wanyama wanaotunyanyasa wana sehemu zao ambazo wakiguswa huumia saana. Mfano ni MAMBA ambaye niliafundishwa kuwa sehemu ya pua ni sehemu ya maumivu saana kwake. Nilikutana na watu walionihakikishia kuona mtu akiachiwa na Mamba baada ya kupigwa puani. Simba huwa ni uoga wa mach na ndio maana hawezi kula kichwa cha mtu, na wale wafao mcho wazi hwa hawatafunwi mno na simba. Tatizo ni kuwa palipo na simba, mla makombo fisi yupo. Kwa hiyo simba akiacha fisi asiye na upungufu huo humalizia.

Candy, hii video haitishi kihivyo. Sekunde za mwanzo wanapom-zoom nyoka ndio inaweza kukutisha lakini anavyoruka inashangaza.
Ila sikwambii uangalie. Unaloweza kufanya ni ku-CLICK PLAY kisha fumba macho mpaka baada ya dk 1 na sekunde 47 kisha fumbua. Lol
Blessings

Born 2 Suffer said...

Mungu mkubwa na anauwezo wake kampa kila kiumbe sifa na nguvu zake.

Yasinta Ngonyani said...

duh! hii kali kweli maana hapo huna jinsi ukikimbia huku naye anakurukia tu. mmmhhh kazi ipo

Bennet said...

Nyoka anayedunga kichwani ni swila (black mamba) rangi ya kijivu kuelekea ya ugolo (brown) anakinywa cheusi tii ndio maana akaitwa blck mamba, ndiye nyoka mwenye sumu kali zaidi, anamwendo kasi zaidi ya nyoka wote (28km/h) kama yuko sehemu mtupieni majani ya mkonge mwitu kwa nafasi ya dakika moja moja, kila utakalorusha ataligonga na kugeuka rangi kuwa njano badala ya kijani, baada ya majani kadhaa ataanguka na kufa

Kifutu au moma ni mpole hang,ti mpaka umkanyage au upekue sehemu aliyopo kwa mikono (hana dawa)

Chatu havamii mtu ambaye si saizi yake na akikukamata vizuri haizidi dakika atakuua kama hukupata msaada, anang'ata hasa mikono ingawa hana sumu ananukia kama waliwali au pilau

Wakijani na anayeruka kama huyu (green mamba) wana sumu kali lakini huuma mara chache wakichokozwa

Sawaka ni jamii ya chatu ila mwenyewe ni mdogo kidogo na hupendelea maeneo chepe chepe, akiwinda ana vurugu sana na ni mbabe, kama unachunga mbuzi akija anakutisha kwanza kwa kutifua vichaka na majani ukikimbia ana kamata anameza

Mija Shija Sayi said...

Bennet, na hawa tunaowaonaga ktk vikundi vya sanaa ni wa aina gani? Na huyu aitwaye Anaconda unamfahamuje? Tunaomba elimu tafadhali.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwa kihaya kuna Nyoka aina ya Nchwera (chwea), nkoraitima (koatima), Nyurubabi (nyaubabi), mpili (pii), njuju (juju)nk