Wednesday, January 6, 2010

Nani "anayewaroga" wasanii wetu?

Q-Chief (shoto) na TID Picha toka Bongo Celebrity
Saida Karoli. Picha toka Last.fm
Oktoba 2 mwaka 2008 niliandika kuhusu UMUHIMU WA WASANII KUWA NA WASHAURI (Bofya hapa) ambapo nilieleza zaidi kuhusu maamuzi wayafanyayo wasanii na namna yaathirivyo OFISI ZAO ambazo ni sanaa wafanyavyo. Niligusia mavazi, maongezi na kwa ujumla nini cha kufanya kuendelea kufanikiwa. Lakini siku zinavyokwenda tunazidi kuona wasanii wanavyojipoteza katika harakati za kujitafuta. Nimesikia wasanii ambao kila atokapo anajaribu aina nyingine ya muziki na pale tunapokaa chini kusema "labda toleo lijalo atarekebisha makosa ya sasa na kuwa bora zaidi", tunakuta msanii huyo kaja na mahadhi mengine na hivyo anakuwa na funzo jingine. Mfano mzuri ni msanii Abubakari Shaaban Katwila ama Q-Chief ambaye kapiga mahadhi mengi na hakuna hata aina moja kati yazo iliyomjengea heshima kwani "hakuna alikomudu kudumu ili kuimudu".

Lakini mifano iko mingi na ULIO WAZI ZAIDI na huyu Dadangu Saida Karoli. Kama kuna wasanii waliodhihirisha ukosefu wa washauri basi ni huyu. Kwa hakika ameonesha kutojua anachokifahamu na kukimudu na kukimbilia ambako hawezi kuwa awavyo. Kwa ufupi SAIDA AMAUKIMBIA U-YEYE NA KUUKIMBILIA U-WAO AMBAO HATAUFIKIA.

Sikiliza nyimbo hizi mbili hapa chini kisha ujiulize ni kipi kilichomsibu mpaka akaacha muziki wa asili aliokuwa akiumudu vema katika lugha aliyoimudu na ambayo ilimfanya kuwa kati ya wasanii waliouza nakala nyingi zaidi za muziki, kwa bei ya juu na kuingiza pato jingi (kwa mkusanyaji). Na ni muziki huohuo wa asili ambao aliimba kwa ufasaha kwa lugha ambayo wengine hawakuielewa, lakini bado walipenda HISIA zake kwenye muziki na walinunua. Kisha akaja "mshauri ama ushauri" wa kuachana na muziki anaoumudu na kujaribu mahadhi mengine. Sijajua upande wa WAPENDWA wengine lakini binafsi nimesikitishwa saana kiwango cha upangiliaji wa muzki, lugha na muziki kwa ujumla. Amepoteza muunganiko wake kwa kutumia muziki duni, lugha asiyo na urahisi wa kuiimba na imekuwa just a mess

Naishia kujiuliza NI NANI "ANAYEWAROGA" WASANII WETU wasijue la kufanya kwa manufaa yao na kazi zao?
Msikilize Saida ktk nyimbo moja ya nyimbo zake za asili. Hii aliiita Mapenzi Kizunguzungu

Kisha sikiliza hii "Reggae sasambua style" yake kuhusu Sweet Tanzania

Blessings

6 comments:

Halil Mnzava said...

Hawana washauri na kama wanao basi pengine hawajui wafanyalo.

Faith S Hilary said...

how about hao "ma-producer" wanaotaka nyimbo itoke na iuzike mitaani...au wasanii wenyewe wakipata "pressure" kwamba watakuwa "one hit wonders"...there are all sorts of things...for example huyo Q-Chief...alitoka na nyimbo zake za "familia"...then sijui akaenda TOP BAND..then sijui ilikuwa taarabu sijui rusha roho ile halafu ss hv mie sijui....all confusing...its hard to remain on "top" in Bongo charts...its what I think

Bennet said...

Muziki wetu unamakosa mengi, msanii mwenyewe utakuta hana shule kama mimi na pia hana exposure, producer nae anahangaika na biti tu wala haangalii msanii kaimba nini na kumrekebisha hata kidogo, mapromota ndio usiseme wao wanangalia ulaji tu

Mija Shija Sayi said...

Saida alikuwa ndo kama Oliver Mutukudzi wetu na yeye huyoo anaondoka, kufika itakuwa ngumu.

Mfalme Mrope said...

kama ulivyosema mzee, tamaa ya uwao inawaponza wasanii wetu. Kuna ulazima gani wa kuimba kiinglish na wakati haukifahamu? Mbali na kushauriwa pia na wanamuziki wenyewe watumie akili zao wenyewe kwani wanajielewa nini wanaweza na nini hawawezi. Usisi una mwanya mkubwa tu wa kutamba kwani nyimbo zinauzika kwa nchi nyingi sana.

nyahbingi worrior. said...

Je!!katika hawa wasanii wetu wakizazi kipya cha bongofleva nitajie hata mmoja ambaye anaimba tungo zenye kuelimisha?

Tungo nyingi nimesheheni mapenzi,sasa tutegemee nini?

Je unaweza kuwalinganisha wasanni wetu na manabii kama Bob,Tosh,Burning,Luciano,Debe,Senzo na wenngine wengi?

Jah naye hubariki tungo za uponyanyi,tungo za haki,tungo za elimi,tungo za kilimo n.k.