Sunday, February 28, 2010

Hawa wote waliwaza "kujitoa mhanga"

Image from Ultimate of Leaders Philosophy Blog
Jumatatu iliyopita Kakangu Profesa Matondo aliandika katika blogu yake akituasa TUWAJENGEE KUMBUKUMBU NZURI WATOTO WETU. Aliandika kwa ufasaha (kama ambavyo amekuwa akifanya mara zote) na kisha akatuachia ka-home work kuwaza tunakumbuka nini kuhusu utoto wetu?
Hakuna asiyekumbuka lolote kuhusu utoto maana ndipo tulipofurahia ama kuchukia maisha. Ni wakati ambao wazazi na walezi walijitoa kwetu ama kutupuuza na hii ni kutokana na nafasi ya utoto katika familia na jamii.
Ni katika kuwaza WAWAZALO WAZAZI NA WATOTO nikakutana na habari hii ya mwanadada ashirikiye michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi inayomalizika huko Canada.
Mdada huyu TUGBA KARADEMIR alionesha upenzi na umudu katika mchezo wa Figure Skating na kwa kuwa ilikuwa ngumu kwake yeye kuendelea akiwa nchini kwao UTURUKI, wazazi wake (Mama akiwa ni Aerospace Engineer na Baba mmiliki wa maduka kadhaa) waliamua kujitoa na kuhamia Canada wakiacha kila walichowekeza maishani mwao nchini Uturuki.Hii yote ni katika kuwekeza katika kile walichoamini mtoto wao anapenda.
UNADHANI WALIWAZA NINI mpaka kufikia hatua hiyo? Waliona taswira gani mbele kuhusu maisha ya mtoto wao mpaka wakaamini ni vema kuwekeza kwake amna hiyo?
Ukitaka kujua ambacho Tugba anakumbuka kuhusu utoto wake na mhanga wa wazazi wake, angalia video hizi hapa chini

Pia wiki hii nimeingia kwenye swali hili hili la WALIWAZA NINI nilipoangalia habari hii iliyotokea huko Oklahoma ambapo kijana aliyekuwa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa kukiuka sheria za usalama barabarani, aliiba gari ya polisi ambaye alisahau kufunga mlango kwa nje na kutimka nalo. Bahati mbaya hakufika mbali akagonga na kukamatwa tena.
Makosa yakaongezeka.
Ninalowaza hapa ni kuwa alifikiria angewaepukaje hawa askari ambao walishakuwa na taarifa zote kumhusu?
ALIWAZA NINI kutaka kukimbia na gari la Polisi? Yasemekana alipopata ajali aliwekwa chini ya ulinzi bila kizngiti licha ya bunduki ya askari aliyekuwa akitumia gari hilo kuwa pembeni yake. Tazama video ya alichofanya hapa chini


***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

1 comment:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ukichunguza vizuri maisha ya hawa "macelebrities" hasa wa kizungu, utakuta kwamba wazazi wao walijitoa mhanga sana mpaka wakafika hapa walipo. Kuna jambo la kujifunza hapa.