Sunday, February 7, 2010

Namjibu Prof. Matondo

Januari 15, Kakangu Prof Matondo aliangika akishangaa kuwa HATA FLORIDA KUMBE KUNA BARAFU!!!(soma mshangao wake hapa). Tena katika maelezo akawa wazi zaidi akisema "Najua Mzee wa Changamoto pengine atacheka tu, lakini mimi hata sikujua la kufanya baada ya kukuta gari limefunikwa na unga wa barafu!". Well, si mmemsoma hapo akisema "unga wa barafu"?

Kisha Kakangu akazungumzia "madhara" ya barafu hiyo akisema BARAFU IMEUA MICHIKICHI YANGU!. Sasa leo naomba kumjibu Kakangu huyu kuwa kilichonichekesha (kama nilicheka) ni huo unga niuonao kwenye picha hapo juu (niliyoinyaka kwenye post yake hiyo) kwani sisi huku huo hauhesabiki kama anguko la barafu, kinachowafanya watu walalamike ni RUNDO kama hili hapa chini. Nasikia sehemu za Canada na u-Scandinavia ndio maisha yao haya. Kwa hiyo kikubwa kwa Kaka Matondo ni kiduuuchu kwangu, na kikubwa kwangu, kuna wengine wanakiona masikhara. Yale yaleeee ya "vijisenti" kwa Chenge ilhali wengine twaona ni mamilioni. Ama kweli DUNIA INA MAMBO
Labda nimpe kakangu ladha ya kilichonikuta leo nikijitumia zaidi ya masaa 4 kusafisha sehemu ya kutokea..
Kaka Matondo, majibu ni haya na video hii hapa chini ni juhudi na karaha za leo. Imenichukua masaa 3 kumaliza kazi. Video kamili ya ka-theluji ketu yaja.
Karibu sana Maryland Kaka

8 comments:

Simon Kitururu said...

Hapo ndio MTU utastukia jinsi tatizo la mtu LIMLIZALO akilitamka liwezavyo kumchekesha mtu .:-(

Ila kwa bahati mbaya kila mtu analisikilizia tatizo kibinafsi kwa hiyo uzito wa tatizo HILOHILO watofautiana kutoka mtu na mtu.

Pole Mzee wa CHANGAMOTO kwa kuhangaika na kitita cha theluji na barafu! Nilipo shughuli yenyewe ndio hiyo!:-)Pole pia Prof Matondo kwa kukerwa vilivyo pia na kiwinta kilichozalisha unga huo!:-)

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Mkodo.
Hii yanikumbusha lileee suala la "VIJISENTI" la Mhe Chenge.
Yaani kile anachokiona Mwalimu Matondo kama SNOW, wenzake twaita "VIJI-SNOW". Sawa na yale MAMILIONI ambayo Mhe Chenge aliyaona kama "VIJISENTI"
Hivi tunastahili kumlaumu Chenge?

Fadhy Mtanga said...

Kwa mimi niliyezowea joto na jua kali la Dasalama nadhani huo unga wa kaka Matondo ningeuona ishu kuliko hata yeye alivyouchukulia.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nadhani Mwanafalsafa Mtakatifu Kitururu ameliweka suala zima katika muktadha fasaha mno na sina cha kuongezea.

Masaa manne ukihangaika na barafu mbona kasheshe? Windshield na madirisha ya gari havipati nyufa na kupasuka?

Kuna kazi kule Washington D.C. nashawishika kuiomba mwaka kesho na kama nikiipata basi tutakaribiana huko huko kwenye barafu. Kazi kweli kweli!

Christian Bwaya said...

Sasa kama Makambako kwa Bongo ndo tunasema baridi, huko kwa Mubelwa patakalika?

Dunia inabadilika kwa kasi mno. Muda si mrefu, tatizo hilo unalokumbana nalo Mube halitakuwepo. Sasa najaribu kufikiri, huko pakishakuwa shwari (kwa maana ya anagalau kuwa kama kwa Profesa Matondo, mitaa ya huku kwetu Ikweta itakuwaje?

Ni akina nani itabidi wahame makwao, sie wa Ikweta, ama nyie wa pembezoni ambamo nako kutakuwa panafurika maji?

Mikutano ya kimataifa imeshindwa kulizungumza kiutatuzi suala hili. Tuchukue hatua za kuzungumzia suala hili kwa wananchi wetu. Twafa jama. Twafa tukizama.

Yasinta Ngonyani said...

Nakumbuka mwaka wa kwanza nilipofika hapa Sweden. ilikuwa ni mwezi wa kumi na mbili na kulikuwa na theluji nyingi kama mwaka huu. Nami nilichofanya nilivaa kkanga na ndala zangu na halifukiT-shirt tu na kutoka nje. Halafu cha ajabu sikusikia baridi. Ila sasa wee! kazi kwelikweli.

Othman Michuzi said...

pole sana kaka na hiyo hali ya huko maana ni noma.

Faith S Hilary said...

LOL! Doh!!! Poleniiiiiii!!!! I hope this doesn't come to us...ikija basi the whole country will be DEAD! DEAD I TELL YOU! (I meant shut down)