Saturday, March 20, 2010

Burudani yarejea...............Asante kwa Da Subi

Doktori mkuu wa blogu hii, Subi binti Wavuti.
Kwa wasomaji wa blogu hii mtakuwa mmetambua kuwa habari nyingi ndani ya blogu hii hukamilishwa na muziki. Ama maelezo ya muziki ama nukuu toka kwenye muziki. Lakini pia kuna VIPENGELE MAALUM ambavyo vyazungumzia muziki ama viko hapa kufikisha ujumbe kupitia muziki.
Lakini kwa bahati mbaya, aliyekuwa host wa muziki wangu (www.imeem.com) alipotea bila taarifa na matokeo yake ni mimi kupoteza nyimbo zooote zilizokuwa zimehifadhiwa huko na hata codes ya zile zilizokuwa zimebandikwa hapa. Hilo liliniathiri na kuathiri "mmalizio" wa habari hapa. Nikaomba radhi na kuanza kusaka mahala pengine pa kutunza na kupata codes za muziki.
Daktari mkuu, fundi mkuu, mshauri mwandamizi na kadhalika na kadhalika wa blogu hii, Dada Subi alisikia kilio chngu na kunionesha mahala ninapoweza kuweka miziki.
Uzuri wa huko (ukilinganisha na niliyokuwa nahifadhia) ni kuwa web ya sasa yakuwezesha kucheza miziki hata kwenye webs ambazo wamefunga mitandao ya kushirikiana (mf Facebook, Youtube n.k)
Vipengele vya I & THEM pamoja na kile cha ZILIPENDWA sasa hivi vina miziki yote iliyopotea. Naendelea kujaza miziki ndani ya post za labels nyingine..
ASANTE SAANA KWA UVUMILIVU WAKO WAKATI WOOOTE NILIOKUWA SINA MUZIKI NA ASANTE SAANA KWA DA SUBI KWA MSAADA USIOISHA
Nakupenda, Nakuthamini na Nakuheshimu sana.
Zaidi ya yote, NAWAOMBEA MEMA WASOMAJI WANGU

8 comments:

Anonymous said...

Siku nilipofika hapa na kukosa muziki na kusoma maelezo yako kuwa iMeem wamehamia MySpace na hata wasitoe taarifa (kwa maana nami nilikuwa na akaunti nao) nilisikitika sana.

Ama kwa lile nililokuelekeza, nikiri kuwa kutokana na udodosi wangu kwenye intaneti, nimeweza kujifunza mengi na kila ninapokumbana na mtu anayehitaji kitu fulani ili kukamilisha hitaji lake ama nikiona mtu anaweza kufaidi kitu fulani ninachokifahamu lakini yeye akawa hafahamu, huwa ninajitahidi kadiri niwezavyo kumwezesha kufanikisha, au kumwomba kufanya ikiwa itakuwa ndani ya uwezo wake. Sichoki kusaidia pale ninapoweza ama ninapowaza naweza kujaribu.

Mubelwa umetufunza jambo muhimu na unaendelea kulirejea kila siku, nalo ni 'kutoa shukrani' wakati wowote. Nimeliona hili na ndiyo maana niliandika posti hii Muhimbili, Mubelwa, Prof Matondo, Yasinta, Kitururu...

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Aksante wajameni...sasa tutamwemwereka vilivyo....lol

Mzee wa Changamoto said...

Kwanza nikushukuru saana Da Subi kwa kunisaidia katika mambo mengi. Umekuwa mmoja wa wengi ambao ninaendelea kufikiria umuhimu wa ku-design na kuwa na P.U.G.U AWARDS kwa ajili yenu.
Ni lazima tukubali kuwa wapo wanaofanya ulimwengu kuwa rahisi na wa furaha na mafanikio kwetu kwa kuwa tu wametushauri ama kutuonesha njia kwa namna moja ama nyingine. Iwe ni kutuonesha kitu ama kutukosoa, ama "kutuzodoa" ama kutufanyia lolote litufanyalo tuwaze kwa undani zaidi na ni yote ni misaada.
Binafsi NISIPOSHUKURU HUWA NAKWAZWA NA NAKUWA NA MZIGO. Najihisi kutaka KUTUA KITU TOKA MOYONI na ninalofahamu ni kuwa yeyote akufanyiaye chochote chema halazimiki kufanya hivyo na anaweza kuamua kukubali adhabu kuliko kukusaidia.
Lakini post hii imenifanya nirejee kujiuliza "where did it all started?"
Sina kumbukumbu na jina la mwalimu, lakini nakumbuka nikiwa SUNDAY SCHOOL (nakumbuka nilikuwa mdooogo kwelikweli) aliingia akiwa na kitabu cha picha. Akaonesha Mama mmoja akisonga ugali. Kisha akasema "huyu mama anafanya nini?" Tukaitikia a"ANAPIKA"
Kisha akauliza "ni wangapi ambao wakipikiwa chakula wasichopenda huwa wanalalamika ama kukasirika ama kuonesha sura ya kusikitika?" Karibu darasa zima lilinyoosha mkono. Kisha akasema "ni wangapi ambao wakipikiwa chakula kitamu kama walivyodhani ama zaidi ya walivyotamani hufurahia?" Karibu darasa zima likanyoosha mikono. Swali la mwisho likawa NI WANGAPI AMBAO WAKIPIKIWA CHAKULA KIBAYA HULALAMIKA NA WAKIPIKIWA KITAMU HUSHUKURU?
Hakuna mkono hata mmoja ulionyanyuka.
Mwalimu akasema "Kama ambavyo tunalalamika tufanyiwapo kibaya, vivyo hivyo tushukuru tutendewapo jema." Akaendelea kusema kuwa wanadamu wanadhani "WEMA NI HAKI KWAO HATA KAMA ALIYETENDA AMEFANYA JAMBO LA ZIADA LAKINI WANADHANI HAWASTAHILI UBAYA WOWOTE HATA KAMA ALIYETENDA AMETENDA KWA BAHATI MBAYA."
Hilo lilibadili mtazamo wangu wa maisha tangu kindergarten mpaka sasa.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Bila Da Subi, mi nisingekuwa na blogu. Karibu kila mwanablogu ameshaguswa na misaada ya mara kwa mara ya kiufundi kutoka kwa Da Subi. Da Subi - USICHOKE kwani kazi yako ni muhimu mno!

ERNEST B. MAKULILO said...

Da Subi ndio fundi mitambo wetu. Ni dada mwenye roho ya upendo na kupenda kuwasaidia watu. Hapendi watu wapatwe na matatizo na wakati yeye anajua tips za kukusaida halafu akae kimya. Mimi binafsi kanisaidia sana ktk blog yangu.Naungana na Kaka Masangu kuwa bila Da Subi asingeweza kuwa na blo....mimi bila Da Subi nisingeweza kuwa na nguvu kubwa ya kuendeleza blog yangu.

Naungana na Mzee wa Changamoto kuwa ni vyema tuanzishe PUGU AWARDS. Mimi binafsi kama zikianzishwa kura yangu inakwenda kwa DA SUBI.

Mungu akupe nguvu zaidi Da Subi. Tunakuombea dada.

MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
San Diego, CA

malkiory said...

Kama walivyoelezea wadau waliotangulia kwa kweli Subi anastahili pongezi ya hali ya juu, ni kwa vile wanablog tumesambaa mno, ingekuwa vema siku moja tukakutana kwa pamoja Tanzania ili tuweze kuwapongeza wadau wote ambao kwa namna moja au nyingine wameweza kutoa mchango mkubwa wa kuelimisha jamii kwa njia ya blogs.Hebu tujitahidi kulifikiria jambo kama hili la kukutana siku moja nyumbani kwetu Tz ili tuweze kuungana na wenzetu waliopo nyumbani.

Sarp said...

shukrani kwa Da Suby

Mija Shija Sayi said...

Da Subi oyeeee! Na mimi nitakutafuta katika suala la muziki kama Kaka mubelwa.

Ubarikiwe.