Sunday, March 21, 2010

Yaaani ni kuwaza tuuu!!!!

"..kila kitu duniani lazima uwaze, hakuna litendekalo bila ya mawazo...". Haya ni maneno ya Da'Mkubwa Lady Jay Dee katika wimbo wake MAWAZO aliomshirikisha Ambwene Yesaya (A.Y)

Na humu alisema mengi kuhusu mawazo kwa wote, ukiwa na pesa, kichaa, mtoto, mkubwa yaani KILA MTU. Hii ina maana wenye kuwaza busara na ujinga pia., wenye kuwaza mema na mabaya vivyo hivyo. Ukweli wa kauli zake waendelea kujidhihirisha kila siku ulimwenguni

Wiki hii nilipokuwa nabarizi vibaraza vya wenzangu KUJIFUNZA hili na lile, nikatua kwa kakangu Prof Matondo akizungumzia POLISI ALIYETUHUMIWA KUTAZAMA VIDEO ZA NGONO KWENYE SIMU YAKE AKIWA KAZINI (Isome hapa) na nikaona ni vema tukaangalia namna watu wanavyotumia vibaya mitandao na kuathiri kazi ama shule.

Lakini kabla hatujaenda huko, wacha nianze na hii ambayo ilikuwa ni WOW!! kubwa kwa wiki nzima.
Image from Catholic Conference of Ohio
Na hii ni habari juu ya mfungwa Lawrence Reynolds Jr wa Ohio ambaye alitakiwa kuuawa kwa sindano ya sumu kutokana na kukutwa na hatia ya mauaji ya Loretta Foster, 67, siku ya Jan. 1, 1994. Lakini kifo chake kiliahirishwa kwa kuwa "hakuwa kwenye hali nzuri kiafya kuuawa". WALIWAZA NINI??
Hii ilitokea baada ya mfungwa huyo kujaribu kujiua kwa kunywa vidonge vingi. Jaribio lake halikufanikiwa na hivyo alikuwa "unconsious enough to be executed". Mmmmmhhhhh!!!
Nilidhani alikuwa anawasaidia kupunguza gharama na taratibu za kumuua, lakini walimhudumia mpaka alipokuwa kwenye hali nzuri kiafya ili auawe. Na ndicho kilichotokea. Lawrence Reynold Jr aliuawa kwa sindano March 9, 2010.
Kwa habari zaidi Bofya hapa
Hii ilikuwa mara ya pili kwa kuuawa kwake kuahirishwa. Mwaka jana, mahakama ya rufaa iliahirisha kuuawa kwa Lawrence kwa kuwa walikuwa wana wasiwasi na utaratibu mzima wa kuwaua wafungwa huko Ohio baada ya mfungwa Romell Broom kuchomekwa sindano mara 18 wakati wakijaribu kutafuta mishipa ya kuweka drip za sumu na baada ya masaa mawili wakashindwa kupata mishipa hivyo kuahirisha uuaji wake. Kwa mujibu wa mahakama, hilo lilikuwa likivunja kile walichosema "Eighth Amendment constitutional rights against cruel and unusual punishment.."
Ili kujikumbusha mkasa huu na mingine ifananayo na hii, BOFYA HAPA
Image from Thinking On The Margin blog
Tukirejea kwenye TEKNOLOJIA, hapa Maryland kuna kesi inayoendelea kuunguruma baada ya wanafunzi 8 wa Winston Churchill High School kutumia kifaa cha kutunza kumbukumbu USB DEVICE "kuiba" taarifa muhimu na za siri (user ID and Password) zitumikazo kuingia katika akaunti ya mwalimu wao na kubadilisha grades zao na za wanafunzi wengine 46. WALIWAZA NINI???
Hili liliathiri wanafunzi wengi kwani majibu ya grades za wanafunzi 700 wa shule hiyo yalikabidhiwa kwa Polisi kwa uchunguzi na ilimlazimu mkuu wa shule hiyo kuwaalika wazazi wote na kuwaarifu kilichotokea. Lakini pia, vyuo vilivyo na wanafunzi toka shule hiyo ambayo ina rekodi ya kufaulisha asilimia 98 ya wanafunzi vilionesha wasiwasi wa usahihi wa wanafunzi wao kuwepo vyuoni mwao.
Soma habari kamili HAPA
Image from iStockphoto
Na mwisho kwa wiki hii ni ilee habari ya askari wa Israeli aliyehukumiwa baada ya kuvujisha taarifa za kina juu ya shambulio la siri lililokuwa likipangwa kufanywa na jeshi la nchi hiyo. Alifanya hivyo kwa kutumia mtandao wa kijamii wa FACEBOOK. ALIWAZA NINI??? Hili la kuwa na uangalifu wa namna tunavyotumia mitandao hii niliwahi kuliandika HAPA.
Matokeo yake ilikuwa ni kuahirishwa kwa shambulio na kupelekwa mbele ya sheria kwa askari huyo.
Soma mkasa kamili wa askari huyo HAPA

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

6 comments:

Faith S Hilary said...

1. Mmh...pole yake...maybe he was just too excited and then he just decided to watch them in order to.........never mind

2. Hakuwa kwenye hali nzuri kiafya kuuwawa? Eh?...this actually made me laugh, you never know labda Mungu kawapangia waendelee kuishi au haikuwa siku yao...lol just a scenario

3. loooooooool 98%???? itabidi wawarudishe darasani kila mwanafunzi since this figure started hahahahhaha!!! so smart yet so dumb!

4. Don't we all just LOVE FACEBOOK? Viva la Facebook! lol

Simon Kitururu said...

MmmH!

EDNA said...

Mmmmmh...hali nzuri ya kiafya kuawa?.... mweee wanataka kumuua tena wanataka awe katika hali nzuri?
Mimi bado sijawaelewa hawa watu.

Yasinta Ngonyani said...

Mawazo!! mmmhhhhh. Jumapili njema na asante kwa wimbo huuu maana ni wimbo ambao huwa nausikiliza sana. Sijui nimewaza nini kusema hivi?

Fadhy Mtanga said...

Kweli waliwaza nini.

Ya mtu kutokuwa na hali nzuri kiafya imeniacha mdomo wazi.

Ya watoto kubadili alama zao, ni wabunifu.

Ila ya Facebook nakosa la kusema maana nami ni walewale! Sijui huwa nawaza nini!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hiyo mawe