Thursday, March 25, 2010

Happy Birthdate Da Agness

Ni sahihi kuwaza, kwani siku zasonga na majukumu yaongezeka
Ni siku nyingine katika maisha ambayo kwa wengine yamaaanisha mengi zaidi. Kuna kumbukumbu nyiingi maishani ambazo kwa wengine zaanza, na wengine zaendelea. Na hiyo ni sehemu ya siku yoyote ambayo kwa wengine ni "special"
Na leo ni siku muhimu kwa Da'Mdogo Agness Anderson amilikiye Blog ya Kiduchu ambaye leo anatimiza mzunguko kamili wa mwaka maishani mwake. Ni "mwaka mpya" wa maisha yake na kama mwana-blog mwenza, napenda kuungana naye katika siku hii muhimu kwake.
Labda kwa kuwa nina tu-miaka kadhaa twa kukabiliana na maisha, nikuase kuwa maisha ya sasa ni ya kukabiliana na kile chema uaminicho. Kwa sasa wapo wengi ambao watajitahidi kuja na "wazo" hili ama lile kukufanya uamini kuwa HUWEZI KUFANYA UTAKALO NA KUWA UPENDAVYO.
Hakuna la kufanya kuweza kuwakimbia hawa watu kwani "wameumbwa wawepo" na ndio ambao husababisha matatizo na UKUAJI wetu maishani. Kwa hiyo katika kuyasaka maisha mahala popote utakapoishi na vyovyote utakavyoishi, Lucky Dube kakukumbusha kuwa "Problems are there left and right. Liars, cheaters, politicians and back stabbers. Making life a little bit more unbearable". Na anaendelea kukuasa kuwa kuna mengi ya kufanikisha maishani iwapo utakuwa makini katika kutumia nafasi njema uzipatazo, kwa usahihi ukikumbuka kuwa huu ni ulimwengu wa kutoa ama kupata, hivyo "you got to take what you can, when you can make the best of it."
Labda kwa kuangalia hali ilivyo sasa, kila mtu anasaka maisha na kila mtu ana taabu zake. Wapo walioshindwa kuwa wema na kufanya ya kusikitisha na kudharau zawadi kuu waliyonayo na MAISHA.
Lakini twaambia kuwa TUZO AMA ZAWADI YA MAISHA UNAYOISHEREHEKA LEO NI ZAIDI YA TATIZO LOLOTE duniani, hivyo "You could be having problems right now, but there's no problem worth your life"
Nakusikilizisha kibao chake Lucky Dube kiitwacho CELEBRATE LIFE (na maneno yake hapo chini) unaposherehekea siku yako hii muhimu
HAPPY BIRTHDATE DA'MDOGO AGGIE

We're living in the world with alot of crazy people.
We're living in the world with psychopaths.
Everyone of them wants to rule the world
Some people have the front row seat
At the top of the world
Some people have nothing but just a life
Problems are there left and right
Liars, cheaters, politicians and back stabbers
Making life a little bit more unbearable
It is a give or take world
So you got to take what you can when you can
Make the best of it. Wow!!

Chorus
say yeah!! Celebrate life
Say year!! Life is good.

We're living in the world with demented people
There's a man standing on the edge of the bridge
Ready to end it all
Some people don't know what life is worth
Some people have the front row seat at the gates of hell
You could be having problems right now
But there's no problem worth your life
People fight to stay alive every day
Cause they know, life is worth more than worries.
So you got to take what you can when can
Make the best of it, Wo!! Ho!! Wo!! Ho!!

Chorus
Say Yeah,yeah celebrate life
Say Yeah, yeah life is good.

Till fade.

4 comments:

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana Da'Kiduchu na uzidi kubarikiwa.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana Da´mdogo Agness. Mungu azidi kukulinda uwe na maisha memma na mafanikio kwa kila ulitendalo.

AGNESS ANDERSON said...

thanx much kaka mpendwa na dada zangu wapenzi YASINTA na DA MIJA kwa kudra zenu... bwana awe nanyi siku zote!

Faith S Hilary said...

Happy Birthday(date) to ya dada wa "kiduchu". God Bless ya n live loooooong!!! hehe! mch luv! xx