Tuesday, March 9, 2010

MIAKA 102, na bado anafanya kazi. Tena JAJI

Image and video from Wesley E. Brown Inn of Court
Wapo wanaopanga mipango miiingi ya namna watakavyostaafu wakiwa na miaka 65 (ama zaidi au pungufu kulingana na sheria za mahala husika). Na pengine nami ni mmoja wao.
Lakini wiki moja iliyopita nilikuwa nasoma kuhusu Jaji Wesley E. Brown wa Wichita, Kansas ambaye ana umri wa miaka 102 na bado anafanya kazi. Yasemekana alianza pilika za maisha akiwa na miaka 10 na mpaka sasa hajaonesha nia ya kuacha kazi. Katika HABARI HII, Jaji Brown amesemwa kuwa katika kazi hiyo kwa miaka 48 sasa chini ya maraisi 10 tangu ateuliwe na Rais John F. Kennedy mwaka 1962.
Amesema hajui atafanya nini atakapoacha kazi kwani amekuwa akifanya kazi maisha yake yote.
Kaka Matondo alishaeleza kuhusu KURUHUSU KIZAZI KINACHOMALIZA MUDA WAKE KITUFUNDISHE KABLA HAKIJATOWEKA na pengine wengi tuaweza kujifuza mengi toka kwa Jaji huyu ili tujue ni vipi ameendelea kufanya kazi kwa miaka 40 tangu atakiwe kustaafu?
Tazama Video yake hapa chini ambayo ilirekodiwa na kuoneshwa miaka 3 iliyopita (alipokuwa na miaka 99)
NB: Larry Hatteberg did the following story on Judge Brown when he was just 99 years old. The lead in is by Daryn Kagan.

Video copyright holders Daryn Kagan (introduction) and Larry Hatteberg (feature).

7 comments:

Fadhy Mtanga said...

Bora huyo anaendelea na kazi yake ya kitaalamu. Hapa Bongo kazi hizo wanastaafu mapema lakini kazi ambayo hawapendi kustaafu ni siasa na hususani kama wanaingia mjengoni.

Mzee wa Changamoto said...

True Kaka.
Si mwamuona mzee nanii mwenye muda mwingi "msinzioni" akiwa mjengoni?
Mie simo

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mh, huyu anaishi muda wa ziada, akistaafu atakuwa kafa tayari. inabidi afe tu akahukumiwe na yeye kama anavyowahukumu wengine

Anonymous said...

Mh! Hukumu ni kazi ya Muumba jamani, lakini kwa umri huu, inabidi amrudie Mola wake na kujitengenezea makazi ya kesho.


disminder.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Pale Mlimani maprofesa wanastaafu mapema kwa mujibu wa sheria halafu wanaendelea kufundisha kwa mikataba mpaka wanazeeka sana. Utaratibu huu huwa unanichanganya.

Godwin Habib Meghji said...

Mimi huu utaratibu wa maprofesa TZ kustaafishwa wakiwa bado wananguvu kabisa za kufanya kazi hauniingii kabisa akilini, haswa kwa nchi yenye maprofesa wachache kama TZ.

Huo utaratibu wa mikataba bora basi ungekuwa wazi. Hauna kanuni yeyote. Nahisi unazingatia zaidi hisia za watu katika kuamua nani aendelee na mkataba nani asiendele

Nakumbuka nilifundishwa hesabu na profesa MASENGE nikiwa UDSM, wakati huo alikuwa amestaafu na anafundisha kwa mkataba. Ukweli alikuwa anaonekana ana nguvu kuliko walimu wengi tu kwenye kitengo cha hesabu. Hapo sijasema uwezo wake wa kufundisha. UKWELI KABISA SIKUWAHI KUFUNDISWA NA MWALIMU YEYOTE HESABU KAMA PROF MASENGE ALIVYOKUWA ANAFANYA. Na hili lilijidhihirisha kwenye matokeo ya mwisho wa muhula. kati ya wanafunzi 25 darasani kwangu 20 walipata A na waliobaki B+.

Nasikitika sisi ndio tulikuwa wa mwisho kufundishwa naye kwa sehemu ya mlimani. Ila nilifarijika kusikia alikuwa anafundisha OPEN.

Mimi sidhani kama unahitaji kuwa kiongozi kutoka taifa lililoendelea kujua kuwa kuna fani watu wanaweza kufanya kazi kwa muda mrefu labda wao wenyewe waombe kustaafu au afya zao kutoruhusu kuendelea

Simon Kitururu said...

Tukumbuke pia kazi inaweza kuwa KILEVI chenye ADDICTION ZAKE kwa mtu.

Nimeshuhudia watu ambao wakistaafu pamoja na kuwa na kipato cha kutosha maisha yanawashinda kabisa wanakuwa hawajui la kufanya kabisa kwa kuwa miaka yao yote tokea asubuhi mpaka jioni yalichukuliwa na kazi zao.


Hawa watu wanaweza kung'ang'ania kazi kwa sababu hiyo tu.

Na kuna watu nimeshuhudia wamevunja mpaka ndoa zao kisa wameanza kukaa muda mrefu nyumbani ndio kutambua hata hawajui MZAZI MWENZA kama walivyokuwa wanafikiri kwa kuwa KI KWELi walikuwa wanakutananaye baada ya kazi tu na sasa kuishi naye kila siku siku nzima WANASTUKIA inasumbua.:-(


Kumbuka kuna watu hawana HOBI na ukiwaondoa katika kazi zao hawajui chakufanya.:-(