Jumatatu ya wiki hii ulimwengu wa reggae ulimpoteza mmoja wa wakongwe huo duniani GREGORY ISAASCS ambaye alifariki nyumbani kwake London kwa saratani ya mapafu (Lungu Cancer). Maradhi hayo aligundulika kuwa nayo mwaka jana.
Nilibahatika kuwa mmoja wa waliohudhuria onesho lake lililofanyika Machi 16, 2008 katika ukumbu wa Zanzibar hapa Washington DC ambapo licha ya kuonekana mdhoofu, bado aliweza kutuburudisha vema kwa nyimbo zake njema zilizompa umaarufu na jina la jukwani la "COOL RULER"
Aliweza kutawala vema jukwaa katika muda wote ambao alitumbuiza na kwa hakika wengi wa wahudhuriaji walionekana kufurahia kazi zake na kama uonavyo hapa chini, tabasamu lilionesha kuridhishwa na uwezo wa mkongwe huyu
KAZI ZAKO ZITADUMU MILELE
1 comment:
PUMZIKA KWA AMANI GREGORY ISAACS!
Nguli pamoja na matatizo yake ya kibinadamu haki yanani simchoki!:-(
R.I.P Nguli COOL RULER!
Post a Comment