Monday, October 25, 2010

Za Kale vs Maisha ya sasa.....MESENJA

Miaka inakwenda na siku mifumo ya maisha inabadilika. Japo si yote ibadilikayo na hata ile ibadilikayo haimaanishi kuwa lazima itabadilika kuelekea kwenye uzuri, lakini kuna mengi ya kukumbuka uangaliapo mfumo wa maisha miongo miwili tu iliyopita.
Enzi za ofisi kufungwa saa sita mchana, enzi za kuwa na msaidizi wa kuunganisha shughuli za kiofisi kama kufuata barua, enzi za kuamini kuwa kuna mwandiko wa kiume na wa kike na mengine mengi ambayo ukiyasikia sasa hayaonekani kuwa na nafasi katika jamii yetu.
Lakini kuna ambalo halijabadilika. Tatizo la baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali kuendekeza mahusiano nje ya ndoa. Na sasa teknolojia ya simu za mkononi na barua pepe vinawawezesha kuendeleza uhuni huo kwa uraisi zaidi. Hii si bahati aliyokuwa nayo Bosi aliyeimbwa na wana Magnet-Tingisha (Bima Lee Orchestra) katika kisa hiki cha Mesenja.
Sikiliza kisa hiki ambacho bado kinaendelea kuitesa jamii yetu kwa baadhi ya "mabosi" wakware kuendeleza uhuni kwa nafasi zao za kiofisi. Pengine kwa wasanii wa sasa waangalie uwezo mkubwa waliouonesha Bima Lee kwa kutumia mapigo yaliyofaa katika kuongea, kuimba na hata kujibizana.
Kazi nzuri sana isiyochuja

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia siku za Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama kupitia mitandao rafiki HAPA na pia kujua tasnia nzima ya muziki na wanamuziki wa Tanzania HAPA

3 comments:

malkiory said...

Mubelwa,asante kwa kuniburudisha na kipande hiki ambacho kimenikumbusha enzi zangu. Huu wimbo haujachuja bado kwasababu ya ujumbe mwanana. Nadhani hapa kuna sauti ya marehemu Eddy Shegi. Kati ya wanamuziki waliopata kutamba Tanzania hakuna sauti inayonivutia kama ya Eddy shegi.

emu-three said...

Du umenikumbusha mbali kweli.Namkumbuka sana mwanamuziki huyu Edy shegy, alikuwa miongoni mwa wanamuziki wenye sauti nzuri!

Yasinta Ngonyani said...

ni ujumbe ambao bado kwa kweli unaendela sijui lini tutabadilika!