Friday, December 10, 2010

Ama kweli......NAMNA UONAVYO TATIZO NDIO TATIZO....Wanawaza nini?

Photo Credits: Huffington Post
Mwanzoni mwa wiki hii, mke wa John Edwards, mgombea urais kwa chama cha Democrat Mama Elizabeth Edwards, alifariki dunia kutokana na maradhi ya saratani. Kifo hicho kilikuja muda mfupi baada ya yeye mwenyewe kueleza nia ya kukatisha matibabu hasa baada ya watabibu kueleza kuwa kulikuwa na nafasi ndogo ya matibabu hayo kuleta uponyaji.
Sasa kanisa moja dogo (ambalo lina ndugu zaidi ya waumini) limerejea tena kwenye ulingo wa habari kwa kutangaza kuwa WATAANDAMANA wakati wa maziko ya Mama Edwards kwa kuwa AMEJIUA KWA KUGOMA KUPATA MATIBABU.
Hili kanisa lijulikanalo kama Westboro Baptist Church ambalo moja ya anwani zake za tovuti (utaona nyingine kwenye press release yao) ni http://www.godhatesfags.com/, lilishafanya maandamano katika mazishi ya Marine Lance Corporal Matthew A. Snyder ambapo kesi ya tukio hilo imefika Mahaka Kuu hapa Marekani.
Ninalowaza ni kuwa WANAWAZA NINI KUFANYA HAYA? WANAITANGAZA VIPI IMANI YAO? WANAHISI AMA KUAMINI VIPI JUU YA UHALALI WA WAFANYAYO???

Hii hapa ni taarifa ya kanisa hilo iliyotolewa kuhusu apingano hayo
Dini hiziiiii. Madhehebu hayaaaaaa.....Kaka KAMALA UPOOOOOO???? ? HEAVEN HELP US ALL!!!!!!!

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

6 comments:

Simon Kitururu said...

Jamaa huwa wananizungua kweli!

Kwa kuwa mara nyingi waendao kuwazingua huwa hawahusiki na walalamikiayo.

Huwa nashangaa wakienda kunyanyasa wazazi wa Marehemu ASKARI kisa alikuwa msenge kabala hajafa. Sasa WAZAZI wa msenge wanastaili vipi kushambuliwa wakati hawakuhusika na usenge?

Sasa wanaenda KUZINGUA kwa Edwards utafikiri wao ndio wanajua HUKUMU ya MUNGU.

Mmmmh!

Mzee wa Changamoto said...

Hapo umenena kaka
Wanapokuwa hai hawaandamaniwi, wakifa ndio waliosalia wanakutana na haya yote
Hii ni dalili kuwa hawa jamaa ni waoga, na wataalamu wa "kuzodoa" wasioweza kuwajibu
AIBU KWAO

Rachel Siwa said...

sasa kwanini wasiandamane kabla hajafa?hizi imani za leo kama mtu kakurupuka usingizini alikuoa anaota!
naona wanahitaji umaarufu zaidi!

Yasinta Ngonyani said...

Binadamu ni wa ajabu sana kwa kweli!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

bwana Yesu asifiwe saaaaaaaana!

emu-three said...

Hujafa hujaumbika, huoni watu wanavyojaa msibani, lakini wakati mtu huyohuyo alipokuwa hai anaumwa watu hawakuonekana! Nawaza kwanini?
Watu wanaonekana baada ya kifo, labda wanakuja kuhakiki, labda wanaonyesha upendo wao wa mwisho , labda...
MSIDHANI nimetoka nje ya mada, ila najaribu kuonanisha imani hizo na tukio lenyewe, kuwa `kwanini alipokuwa hai hayo hayakutendeka..?