Sunday, December 19, 2010

Ni kweli twakusanya vya kale...Ila $90K kwa jeneza lililotumika??? Mmmmhhhhh!!!

Photo Credit: World News Insight
Dunia ina mambo yake. Na kuyashangaa, kuyapenda, kuyachukia ama kuyaona mazuri ama mabaya itategemea na upande uyaangaliayo.
Yaani yategemea uko wapi, waangalia mambo kwa jicho gani na hili laweza kukufanya ukaona mtu katenda jambo la maana ama la.
Duniani kuna watu ambao wanafanya kazi ya kukusanya vitu hasa vya zamani, maarufu na ambavyo ni "adimu".
Si mlisikia mnada wa glovu ya Michael Jackson? Na wengine (kama mfanyakazi mwenzangu) hukusanya pesa za mataifa mbalimbali, mwingine anakusanya vikombe vidogo vya "shot" vyenye nembo ama majina ya nchi mbalimbali
Wiki hii kuna "mkusanyaji" mmoja ambaye hakupenda kujulikana amenunua lililokuwa jeneza la mtuhumiwa wa mauaji ya Rais Kennedy wa Marekani kwa zaidi ya dola 90,000.
Jeneza hilo la "kawaida" ambalo lilikuwa na mwili wa Lee Harvey Osward kwa miaka 20 kabla ya "kuzikuliwa" kwa uchunguzi na kuzikwa upya kwenye jeneza jipya, limeharibiwa kutokana na unyevu na maji kwa miaka ambayo lilikaa na mwili kaburini, liliingizwa mnadani wiki mbili zilizopita.
Kuna mitumba ya kununua, lakini mtumba wa jeneza???
Angalia mwenyewe video hii inayoeleza kwa zaidi.

Ninalowaza hapa ni kuwa aliyenunua "jeneza la mtumba" ALIWAZA NINI?

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Sidahani kama waliwaza kitu mimi ningefikiria kuvirigiwa mpasa/mkeka! Jeneza la MTUMBA KAAZI KWELIKWELI