Friday, March 4, 2011

Them, I & Them...ECHO OF MY MIND....Luciano

Photo Credits:Yahoo Sports
Juni 26, 2009 niliandika bandiko kwenye kipengele hikihiki nikimmzungumzia HASHEEM THABEET alipopata nafasi ya kuingia kwenye ligi yenye kufahamika zaidi katika mpira wa kikapu duniani ya NBA (Irejee hapa) na kubwa nililoandika ni namna ambavyo ALIFUATA MWANGWI WA FIKRA ZAKE na kujiunga na ligi hiyo licha ya tetesi ama minong'ono ya wengi kwamba hakuwa tayari kwa ligi hiyo.
Miaka karibu miwili baadae, hali si kama ambavyo tungependa kuiona katika rekodi za Hasheem Thabeet kwenye mpira wa kikapu. Takwimu zinaonyesha kuwa ana wastani wa kufunga pointi 1.2 kwa mchezo, anapata rebound kwa wastani wa 1.6 kwa mchezo na kusaidia kufunga kwa wastani wa 0.1 kwa mchezo. Na Ijumaa iliyopita (Februari 24, 2011) ametangazwa kuhamishiwa Houston Rockets katika mabadilishano muhimu ya kimchezo baina ya Menphis na Houston. Wengi wamezungumzia na kutoa maoni mbalimbali. Wapo wanaoamini kuwa HAKUPEWA MUDA WA KUTOSHA KUFANYA MAZOEZI, wapo wanaoamini kuwa ni nafasi ya kujijenga kimchezo, wengine wanadhani anahitaji kocha binafsi wa kumsaidia katika kipindi ambacho wako kwenye mapumziko na mengine mengi.
Lakini wengi wanakubali kuwa HASHEEM ANA KIPAJI. Na kama hivyo ndivyo basi kwanini ameshuka namna alivyoshuka?
Watu wana maoni tofauti na mawazo mchanganyiko juu ya Hasheem. Nilipokuwa napitia UKURASA HUU WA YAHOO SPORTS nikakutana na maoni ya watu mbalimbali ambayo yamenifanya nirejee wimbo huu siku ya leo kama USHAURI kwa Kaka Mdogo Hasheem
Mmiliki huyo amesema anaona kila sababu na dalili kuwa Hasheem anaweza kuwa mchezaji bora zaidi katika ligi hii na hilo wanaweza kuja kujutia miaka ijayo. Nanukuu alivyosema kuwa " ... I think Houston needs a good center and I think that Thabeet could come back to haunt us. ... Absolutely, it's hard for us (to trade Thabeet). It's extremely hard. ... If he develops, he's going to be a big factor in this league and we might be eating our words."
Yote ju ya yote, napenda kurejea nililosema mwanzo kabisa wakati akijiandaa kuingia katika ligi hii, kwamba HASHEEM ANASTAHILI KUJIPANGA UPYA, KUWA NA WASHAURI WA MCHEZO NA MAISHA na KUTAMBUA KUWA MAISHA YAKE NI MCHEZO NA ANASTAHILI KUWEKEZA HUKO.
Hasheem ANASTAHILI KUWA MAKINI NA WALE WAMZUNGUKAO kwani hao wana athari kubwa saana katika mawazo na maneno ambayo yanachangia katika maamuzi yake ambayo nayo huchangia katika maisha yajayo katika mchezo na nje ya mchezo.
Ni wakati ambao anastahili KUTAFAKARI NJIA SAHIHI YA MCHEZO WAKE NA KUSIKILIZA MWANGI UTAKAOMPELEKA PEMA.
Hii yaweza kuhusisha kujitenga na marafiki wasio na mtazamo sawa na wenye maendeleo katika mchezo (ambao ni kazi) na maisha kwa ujumla.
Mimi ninasema, lakini NI UAMUZI WA HASHEEM KUSIKILIZA "ECHOS OF HIS MINDS"
Msikilize Luciano katika kibao chake ECHOS OF MY MIND

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Simon Kitururu said...

Mie namtakia tu kila lakheri!

Rachel Siwa said...

Nami pia namtakia mafanikio mema!