Tuesday, April 5, 2011

Labda swali si YANINI, bali KWANINI YANINI??

Hivi karibuni nimebahatika kupata barua pepe mbili kutoka kwa wasomaji wa Changamoto Yetu. Ya kwanza toka kwa msomaji "msiri" ambaye (kwa mujibu wa barua pepe yake)amekuwa mfuatiliaji mzuri wa mabandiko, na nyingine kutoka kwa mtu ambaye aliniuliza swali lililonifanya kumjibu haya niandikayo sasa. Msomaji wa pili aliniuliza "hivi unanufaika na nini kwa kuwa na blogu? Blogu yako hasa ni YANINI?" Hilo lilinifurahisha sana kwani mara zote "NIMESHINDWA KUACHA KU-BLOGU KWA SABABU YA SABABU YA KUANZA KU-BLOG". Na kwa huyu NDUGU kuniuliza hivi alirejesha fikra nzima ya KWANINI NILIANZA KU-BLOG? Nirejee kusema kuwa BLOGU HII ITAKUWA NA INAANDIKA MAMBO AMBAYO KAMA HAYATAFUTIWI UFUMBUZI, YATAENDELEA KUWA NA MAANA AMA CHANGAMOTO YAKE HATA BAADA YA MIAKA KADHAA KUPITA. Ndivyo nilivyoamua kufanya. KUTOTOA TAARIFA BALI KULETA CHANGAMOTO. Na hili ndilo nililofanya tangu post yangu ya kwanza (baada ya POST HII) ambayo ilizungumza ama kuleta changamoto kutokana na kile nilichoona. Na kwa kuwa mpaka sasa bado hakijashughulikiwa, CHANGAMOTO HIZI BADO ZIKO HAI LEO HII, KAMA AMBAVYO ZILIKUWA Agosti 25, mwaka 2008 nilipoiandika. Ndio maana nilipomaliza kujadiliana NIKAMWAMBIA "SWALI SI blogu ni YANINI, bali KWANINI anawaza ni YANINI" Hapa chini ni post hiyo ya pili kuwa posted hapa CHANGAMOTO YETU.

Monday, August 25, 2008
Olimpiki imeisha. Tumejifunza kitu? Michuano ya Olimpiki ndio imemalizika na pamoja na kupambwa na kupambika kwa sherehe za kufungua na kuhitimisha michuano hiyo, bado kuna maswali ambayo wapenda michezo wengi wanaendelea kujiuliza. Wapo wajiulizao kama kuna nchi yoyote ambayo itajaribu kufanya "sherehe za kufuru" kama walivyofanya waChina na kuna ambao wanaendelea mbele zaidi kuangalia jinsi watu walivyoweza kuvunhja rekodi mbalimbali na kujiweka pamoja na kuziweka nchi zao kwenye ramani ya michezo. Na hapo ndipo nami ninapogota, nikiangalia mafanikio ya nchi mbalimbali katika michezo mbalimbali nikarejesha mawazo hayohayo kwa nchi niipendayo na kuithamini TANZANIA, najikuta nakwazwa na maswali kadhaa. Pengine michezo kama kuogelea itatugharimu saana maana waogeleaji wa kimataifa waliofanya vema wanawekeza gharama kubwa saana kwenye mchezo huo kuanzia chakula mpaka mazoezi. Lakini pia kuna sehemu nyingine ambazo naamini tungestahili kufanya vema kiasi. Hivi ni kweli kwamba Tanzania hatuna wakimbiaji wazuri? Na iweje kwa jamii kama ya Kenya ambayo tumepakana nayo na tunashabihiana kwa mambo mengi (hasa ukanda wa kaskazini upakanao nao) wanaweza kufanya vizuri katika michezo kama mbio ndefu nasi tushindwe? Hivi ni kweli kuwa hatuna wapiganaji wenye vipaji vya kuweza kufanya vema kwenye michuano kama hii? Vipi kuhusu walenga shabaha? Sina takwimu lakini nakumbuka kuwa walikuwepo wenye vipaji katika nyanja nyingi za michezo (hasa mikoani nilikosomea) tena wengine wakifanya vema saaana hata katika michezo ya mashule kama Umisseta lakini wanapomaliza shule hakuna utaratibu mpango mahususi wa kuwaonesha njia kuelekea kwenye mafanikio na ndio maana wanaishia kuacha kushiriki michezo na kujiingiza kwenye kazi za kusukuma siku kama uvuvi, ukulima na muda mfupi baadae kwenye ujenzi wa familia. Kwangu mimi nadhani kuna pengo kubwa kati ya serikali, jamii na michezo. Kwa SERIKALI utoweka thamani halisi ya michezo na hata kutoitengenezea njia sahihi ya kuwawezesha wale wenye vipaji halisi waweze kujikita huko na kujiajiri kwa manufaa yao, familia zao na taifa kwa ujumla. Pia JAMII lazima itambue kuwa namna nyingine ya kujiajiri katika michezo ni kupitia elimu. Tumesikia baadhi ya washindi (kama Kirsty Coventry wa Zimbabwe) wakisema namna walivyoamua kujiunga na vyuo vitoavyo scolarship nje ya nchi zao ili kupata vifaa, wakufunzi na mazingirz bora ya kufanya vema katika michezo waipendayo. Tunao kina Hashim Thabit ambao mchezo ni sehemu kuwa ya mwendelezo wake kielimu, lakini twahitaji wengi wenye kujijua vipaji vyao kusaka mazingira mema nje ya nchi ili waweze kujianda na kuwa katika viwango vya kimataifa kisha warejee nyumbani kunyanyua mazingira ya mazoezi kwa waliokosa nafasi ya kuelekea waliko. Na MICHEZO ama taasisi za michezo ziache kuendeshwa kama mali za kina fulani. Ubadhirifu kwenye vyama na mashirikisho kimekuwa chanzo kikubwa cha kushindwa kupata washiriki wanaostahili na pia kuigeuza Dar Es Salaam kama ndio Tanzania kunanyima walio na vipaji halisi nje ya Dar kutuwakilisha na matokeo yake tunaishia kuwa washiriki na si washindani achilia mbali washindi. Ni CHANGAMOTO YETU sote kufikiri namna ya kutatua yaliyotukwamisha mwaka huu, ili tujwe tunakotaka kuwa katika Olimpiki zijazo huko London. Posted by Mzee wa Changamoto at 1:02 PM Labels: Sports

3 comments:

heel pain said...

Find everything you need to know about Fungal Nails Infection including heel pain, Sports Podiatry and orthotics Visit Melbourne Podiatrist and get rid of that pain in your lower limbs and feet. At Melbourne Podiatrist, we help you improve your quality of life.

emu-three said...

Na kwanini uulize ya nini? ya nini kwanini? Oh mkuu nabakia kujiuliza maswali mengi na kuwaza mengi.
Huyu muulizaji labda ningemuuliza kwanini watu wanatunga vitabu? ni swali ataliona halioani na swali lake, lakini kwangu mimi blog ni sawa na kitabu, lakini blog imeenda mabli ziaid kwasababu inakupa nafasi ya kujadili `nusu ya moja kwa moja' na wengine inakuwa `moja kwa moja.
Blog ni uwanja mpana kwani unaweza kupata vitu `bure' ukajifunza, ukaelimika, na kila mmoja anapata uhuru wa kutoa kile akiwazacho.
Kuna usemi usemao, `elimu yako ni dhahabu, lakini dhahabu hiyo haitakuwa na maana kama utaifukia, ili elimu yako iwe na faida, itoe kwa watu..ifanyie kazi...basi kublogi kunasaidia wengi wetu ambao tulikuwa na kitu , na tunataka wengine wakipate, na tulikuwa hatuna njia nyingine huria, hii njia imetupa nafasi hiyo!
Huenda mwenye blog akawa anapoteza muda mwingi sana, lakini ni bora kuhangaika hivyo kuliko `kuifukia ile elimu yake aliyoipata'
Ni hayo tu mkuu

Rachel Siwa said...

Sababu au jibu pia lipo, ndiyo maana naye akabahatika kuingia na kuchangia,Pia kaleta changamoto kwako kaka Mubelwa,kwa wasomaji na yeye pia. Ndiyo akaguswa kukuuiliza!!
Asante kwa Swali lako mpendwa mana kama kaka asinge blog usingeweza pakupata kuuliza swali lako na kuuliza si ujimga ni kujifunza!.