Sunday, May 1, 2011

Waliwaza nini kutenda waliyotenda baada ya kutenda waliyowaza?

Photo Credit: Kinesis Marketing
Niliposoma haya matukio nikawaza WALIYOWAZA mpaka KUTENDA haya baada ya kuwa WAMETENDA WALIYOWAZA AWALI.
Hii ni kuhusu "watu" hawa ambao kwa fikra zilizofuata baada ya MATENDO yao wameufanya ulimwengu kuwaza WALIWAZA NINI?Tuanze na "jirani" zangu wa Pennsylvania ambapo watu wawili "walifanikiwa" kuiba toolbox nyumbani mwa mtu na bila kuchelewa wakaamua kwenda kuliuza "fastafasta". Ambalo hawakuwaza ni "wapi pa kuliuza" na matokeo yake ni kuwa wakajikuta wanaenda kazini kwa waliyemuibia na kujaribu kumuuzia. Mwenye mali alipoangalia vema, akafananisha na toolbox yake, lakini akasubiri mpaka alipofika nyumbani ambako aligundua kuwa AMEIBIWA. Polisi waliwakamata Cody Lee Littrell (32), wa Hanover, Rebecca Erinn Dice mwenye miaka 32. Habari kamili waweza kuisoma HAPA.
Leo bado niko na WAHALIFU tuuu. Tumzungumzie huyu mwingine, Christian Longo, ambaye ANATAKA KUREJESHA IMANI YAKE KWA WANAJAMII baada ya kuua mke na watoto wake watatu.
Photo Credits: NY Dailynews.com
Sasa analazimisha serikali kumkubalia kutoa viungo vyake ili vikasaidie kuokoa maisha ya watu wengine baada ya kuuawa kwa sumu. Kwa mujibu wa ukurasa huu wa MSNBC.COM, "Christian Longo, 37, says he wants to do more to take responsibility for killing his family and dumping their bodies in coastal bays nearly a decade ago than simply accepting execution by lethal injection." Yaani anawaza KUOKOA maisha ya mtu mmoja baada ya kuwa ameua wanne. ANAWAZA NINI?
Najua wengine wanaisoma hii kupitia FACEBOOK. Basi kwanza nikukumbushe nilichowahi kuandika kuhusu mitandao hii ya kijamii. Niliandika kuhusu "kisa cha mama mmoja ambaye amepoteza mafao yake baada ya taswira katika ukurasa wake wa facebook kumuonesha mwenye furaha kuliko alivyoandikishwa kazini. Hiki ni kisa cha kweli na mama huyo sasa anajuta kwa kuwa na picha hizo ambazo zimetibua malengo yake a maisha.
Unaweza kufuatilia kisa kamili HAPA . Sasa wiki hii nimesoma kuhusu hawa wengine ambao "walifanikiwa" kuiba dola 62,000 benki, kisha wakaenda kujigamba kwenye Facebook, jambo lililowarahisishia polisi kazi ya kuwanasa. Jamaa hao waliandika kwenye Facebook siku moja kabla ya kwenda kuiba kwamba "U HAVE TO PAST THE LINE SOMETIMES!! TO GET DIS MONEY!!" kisha kesho yake baada ya "mafanikio" ya uporaji huo, mmoja wao akaandika "I'M RICH (expletive)." Haikuchukua muda kwa wao kukamatwa na kukiri kutenda kosa. WALIWAZA NINI? Soma kisa kamili kilichowashangaza hata maafisa wa FBI HAPA .
Na mwisho ni HUYU "mheshimiwa" ambaye alifanya kazi ya ziada juu ya kazi ya ziada kupunguza kazi ya ziada ya kumsaka. Photo Credit: Daily Mail
Ninamzungumzia Anthony Garcia wa California ambaye baada ya mauaji aliyofanya kwenye duka moja la pombe, alienda na kuchora tatoo kifuani mwake inayoonyesha eneo zima la mauaji lilivyotokea mwaka 2004. Sasa Garcia ambaye ni mwanachama wa kundi hilo la Rivera 13, anakabiliwa na kifungo cha miaka 65. Hebu soma kwa undani habari yake HAPA.
Kwa hawa wote...nawaza kuwa WALIWAZA NINI kutenda ama kutaka kutenda haya baada ya kuwa wamewaza waliyotenda awali?
NAWAZA KWA SAUTI TUUUUU!!!!!!!!!!!!!!!

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

1 comment:

emu-three said...

Waliwaza katika giza lilogubika ubongo wao, na mwanga ulipotokea wakashindwa kujiamini kuwa kweli mimi nilifanya haya niliyokuwa nimewaza...nyongeza tu mkuu