Sunday, June 12, 2011

Labda ni sisi wa kubadilika, sio wao.Lakiniiii..........

MAANDISHI HAYA "YATALALIA" KWENYE NUKUU MBILI.
Ya kwanza ni ile ya Lynn Hall isemayo "We did not change as we grew older; we just became more clearly ourselves". Na ya pili ni ile ya Jeremy Taylor (1613 - 1667) isemayo "It is impossible to make people understand their ignorance; for it requires knowledge to perceive it and therefore he that can perceive it hath it not."
Siku za karibuni kumekuwa na MANENO kadhaa kuhusu mshiriki aliyetoka kwenye JUMBA la Big Brother Africa. Well!!! KWA MARA NYINGINE. Na safari hii maneno yametokana na baadhi ya vitendo vya mshiriki wa mwaka huu MWENYE ASILI YA TANZANIA Bhoke Egina vilivyoonekana kwenye mitandao mbalimbali.
Lakini tukirejea nyuma kidogo, tutaona kuwa HAKUNA MSHIRIKI AMBAYE HAKUTOKA NA "MAANDAMANO YA HABARI" kuhusiana na uwepo wake jumbani humo. Labda HAKUNA ALIYESTAHILI KUTOKA BILA HABARI (kwa kuwa jengo lenyewe limewekwa ili kuvutia habari na hasa udaku), lakini aina ya habari ndizo zinazoleta shida hapa.
Kaka wa kwanza kuingia humo, Mwisho Mwampamba alitoka na yake. Mwisho akipokelewa alipotoka BBA
Yalikuwa ni mchanganyiko wa aliyotenda na yaliyofuata. Mshindi wa mwaka uliofuata alikuwa Richard Bezuidenhout.
Richard akishangilia ushindi wake
Kama kawaida, naye tulisikia mshikemshike wake na mkewe na wengine. Yooote kutokana na yaliyotendeka humo. Lakini alirejea na "kitita" kwa hiyo yapo "yaliyosameheka".
Kisha akaja mwanadada Latoya Lyakurwa ambaye naye alifanya yake. Aliporejea hakuwa kimya, katika mahojiano yake niliyoyaweka kwenye makala hii hapa, aliwaasa wananchi na waTanzania kufunguka akili zao na kutambua kuwa hii ni "new era" ambapo hatuishi kwenye miti na wala hatuvai majani hivyo inatupasa kukubali kile tunachokiona kwenye Televisheni. Akijibu swali la mwandishi aliyemuuliza anaonaje ama juu ya wale wanaosema kuwa Big Brother haiendani na mila na tamaduni za wa-Tanzania na waAfrika? alisema "... mimi nasema watu wafunguke akili. Utandawazi, yani ni kwamba (kicheko) nilikuwa nataka tu niwaambie kwamba yaani wafunguke mawazo yao yaani kwamba sasa hivi hii ni new era, yaani tuko katika maisha mapya hatuishi tena kwenye miti, hatuvai majani, kwa hiyo hata kuangalia vitu kama hivyo kwenye Tv inabidi tu-accept, kwa hiyo it's a new era, kwa hiyo tufungue akili zetu na tujue kwamba huu ni utandawazi"
Kisha akaenda Kaka Steve Kanumba Kanumba alipoalikwa kukaa ndani ya jumba la Big Brother Africa kwa siku chache
Yeye (ambaye hakwenda kama mshiriki wa Tanzania bali kama nyota na kwa muda mfupi) HAKUFANYA jambo baya ama la kusikitisha, lakini bado watu wakasema hakuzungumza KIINGEREZA vema. "Wakamlima". Nami sikusita kumtetea hapa. Nililoamini (kama nilivyoandika ni kuwa kama Kanumba anawakilisha mamilioni ya vijana wa kiTanzania ambao wana elimu kama yake, unadhani unaweza kumuweka na vijana wangapi ambao wataweza kukaa nyuma ya Camera na kuongea kama alivyoongea??? Na pengine kwa mazingira aliyosomea, kukulia na hata afanyiayo kazi, tulitaraji Kanumba awe na kingereza cha kiwango gani?? Mbona tupo wengi wenye kiwango hicho na tunawaona wengi hata nchi za nje (kama hapa Marekani) ambao wametoka kwao (mfano waMexico) na kuishi hapa miongo kadhaa na bado hawezi kuunganisha sentensi? Ni kweli kuwa Kanumba kafanya vibaya namna hiyo na si kwamba kuna sababu ya ziada kumshambulia? Anyway...Tuachane naye.
Mwaka jana ilikuwa ni "walewale" nami sikusikia mengi mpaka mwaka huu ambapo yaonekana dadetu "kafunika bovu" huko. Bhoke Egina
Nami nilikuwa nasubiri atakachotueleza punde atakapotua maana nilishasoma maswali kabla hata hajatoka. Na yeye alipofka hakusita kusema kwa wanaomfuatilia kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa “what’s a big deal”?
Kisha akasema HAKUIWAKILISHA TANZANIA, na pia hakuwa amebeba bendera ya taifa. Msikilize ukimtazama hapa

Labda ni sisi tusiojua kama anayeenda huko ni mwakilishi wa uTanzania, mwakilishi wa Tanzania ama mwakilishi mwenye asili ya Tanzania na kwa kutokujua hilo tunakosa kujua kama anatuwakilisha sisi ama anafanya afanyayo kwa utofauti nasi japo tuna asili moja.
Labda ni sisitusiojua mchezo halisi wa Big Brother Africa na ndio maana tunalalamika kuwa ni “nje ya maadili” yetu. Pengine wanayofanya ni SEHEMU YA MCHEZO na miongoni mwa mambo waliyokubaliana baina ya waongozaji na washiriki na yanayotokea ni mambo ambayo sisi kama jamii tuna uhuru wa kuangalia ama la.
Labda ni sisi tusiojua tabia halisi za washiriki na kuwatuma “wakatuwakilishe” kwa tabia tunazoamini tunazijua. Na wakifika huko “wakawa walivyo” (kama alivyosema Da Bhoke,) tunalalamika kuwa wametenda tofauti na tunavyotaka wawe. Kwa kuwa hatukufanya “homework” yetu kuwajua.
Labda ni sisi tunaopenda kuangalia yale yanayotukera hata kama hatulazimiki kufanya hivyo. Kisha tunayatangaza kwa kulalamika kuwa ni uchafu huku tukihimiza anayetaka kuona ‘uchafu’ huo aendele mahala fulani bila kujua kuwa kwa kufanya hivyo tunatangaza “uchafu” huo.
Ukisikiliza katika video hii ifuatayo, (dk 2:30) utasikia Dina akiuliza kuhusu kupimwa kwa washiriki kabla ya kuingia mle ndani “hata yale magonjwa makubwa makubwa”. La labda swali ni kama watazamaji wanajua ni kwanini wanapimwa? Kama wanajua kuwa moja kati ya “matarajio” ya kwenye Big Brother ni kufanya mapenzi? Na kama suala la mapenzi haliko katika “rada” za mchezo, ni kwanini wapimwe? Na kama mchezo umelenga kwenye “kuchangamana” na kujua mambo mbalimbali kuhusu nchi mbalimbali (bila kufanya mapenzi) kuna mafunzo yoyote ya kinga ya mapenzi na maradhi yanayotolewa?

Ninaloamini ni kuwa
NI SISI TUSIOULIZA KABLA YA KUANDAA "WASHIRIKI / WAWAKILISHI" WANAOKWENDA HUKO. Na ndio maana hata baada ya Bhoke kusema hakuwa mwakilishi wa Tanzania, sikusoma, kusikia wala kutazama popote ambapo mwandishi alimuuliza mwakilishi wa M-NET kwamba Bhoke alienda Big Brother kama nani?
SI SISI WALA WAO ANAYEJUA JUKUMU LETU, HIVYO KWA KUTOTIMIZA WAJIBU WETU TUNABAKI KUNYOSHEANA VIDOLE.
Labda ni sisi wa kubadilika. Lakiniiiiii......wao (washiriki) si ni sehemu ya sisi (jamii)? Na tukibadfilika sisi si tutabadili "wao wajao"? Pengine badiliko la kwanza ni sisi kutambua kuwa WATU HUJIDHIHIRISHA U-WAO (kumbuka nukuu ya kwanza yake Lynn Hall isemayo "We did not change as we grew older; we just became more clearly ourselves.") hasa wanapokuwa "nje ya kwetu" japokuwa wanasahau kuwa TEKNOLOJIA YA SASA INATUTENGA KWA KUTUWEKA KARIBU NA KUTUWEKA PAMOJA / KARIBU KWA KUTUTENGA.
Namalizia na nukuu ya Jeremy Taylor (1613 - 1667) isemayo "It is impossible to make people understand their ignorance; for it requires knowledge to perceive it and therefore he that can perceive it hath it not."
Na huu ni MTAZAMO WANGU kwa namna nionavyo tatizo, LABDA NAMNA NIONAVYO TATIZO NDIO TATIZO.

1 comment:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aliwajibu vyema, hakwenda kuiwakilisha TZ wala U-TZ kama TZ yenyewe na U-TZ vina uhalisia

ni wakati wa kuongeza ushenzi vichwani mwa watazamaji ili muwe wapole kama kondoo