Friday, June 17, 2011

Them, I &Them. MAXI PRIEST ......... Cry For The Children

Jana ilikuwa SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.
Siku ambayo ilianza kuadhimishwa mwaka 1991, inathamini UJASIRI wa watoto wa Soweto nchini Afrika Kusini ambao June 16, 1976 waliandamana kutaka ubora zaidi katika elimu na pia kufundishwa kwa lugha ya kwao. Lakini sasa, matatizo ya mtoto wa Afrika ni zaidi ya hayo. Kila uchao ni vita, kuuawa, kubakwa, kutelekezwa, kulelewa na mzazi mmoja na pengine mlezi kwa kuwa baba na mama hawapo. Elimu duni, malezi kwa wadogo zao na mengine mengi.
Kwa baadhi ya watu HUU NI KAMA MFUMO WA MAISHA.
Lakini haitakiwi kuwa hivi. Na ZAIDI NI VITA AMBAVYO VINAWAUA WATOTO WENGI WASIOJUA NINI NA KIPI KILICHOSABABISHA YANAYOENDELEA.
"Slow down everyone pay attention let us reason for awhile, I'm worried about this everyday killing that is turning into style. Don't try to convince its normal, playing with human lives. I Don't know about you but I know its brings tears to my eyes.
Ndivyo anavyoanza hivyo Maxi Priest kwenye wimbo wake huo unaozungumzia athari za vita kwa watoto na Mama zao. Ni mambo ambayo tunaona yanaendelea sehemu nyingi ulimwenguni ambako watoto wasiojua hili wala lile kuhusu vita wanalazimika kukimbia kila dakika kusalimisha maisha yao. Ni maisha hayo ambayo anayawakilisha kwa wahusika kuwa kuwauliza wafikiriacho kwa kuwa yeye sio tu analia, bali anaomba kuwa sala zijibiwe wawe huru kama asemavyo "And I cry for the childrenAnd I pray for themThat someday consciousness will once againBe the answer to our prayers "

ABC Image
Lakini Maxi ameanza kwa swali kwa viongozi wanaojitahidi kuifanya vita kama sehemu ya maisha tunayotakiwa tuikubali, na sasa anaendelea kuwauliza juu ya uwezekano wa siku tutakayoamka na kuliona jua bila hofu ya maovu na hujuma akiuliza "How many more lives do you need for your game? Cause we're counting. How many more mothers will you leave in pain?
Cause it's mounting. Could you give me a time or a day, how much longer will we have to wait, will there be sunshine and no trace of crime when I wake? Now I'm tired"
BBC Image
Ni "uchovu wa kuona maovu" alionao Maxi ambao kila mmoja anaushuhudia sasa hivi kwa watoto kugeuzwa chambo cha mauaji ya wakatili wachache wanaotaka kutawala na kusahau wao ni nani na wanawafanyia ukatili kina nani. Kupoteza utu wao kwa kusaka ubora na uimara wa maovu yao na hapa anasisitiza kuwa "Now I'm tired of all the goings on around us everyday. How did the little bitty innocent babies become pray, and by the way how could we allow ourselves to go so far, I'm almost certain we've forgotten who we are, I'm wide awake in a dream that never ends, and my heart cries out for help everyday".
Sina la ziada kwa kazi aliyoifanya Maxi Priest hapa. Ni AMANI, HESHIMA NA UPENDO na kwa hakika ndivyo Maxi Priest na kundi lake (THEM) wanavyoelezea hayo ambayo mimi (I) nimeyaona na kuyaweka kwa wahusika (THEM)

Waweza kujua zaidi juu ya Maxi kwa kubofya http://www.maxipriest.com/index2.htm . Bofya player hapa chini kusikiliza ujumbe mzito wake Maxi.

BLESSINGS

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

No comments: