Sunday, July 31, 2011

RAMADHAN NJEMA NDUGU ZETU

Kwa siku kadhaa zilizopita, asilimia kubwa ya takribani watu Bilioni moja waumini wa dini ya Islamu wamekuwa wakijiandaa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa tisa na MTUKUFU zaidi katika kalenda ya kiIslamu.
Mwezi huu uambatanao na mafunzo na njia sahihi za kuishi kiIMANI, na uwe nguzo ya maisha yetu hata baada ya kumalizika kwa mwezi huu
Yafunzwayo na kuhimizwa kwenye mfungo na mwezi mzima, ni mambo ambayo naweza kuyaita NJIA SAHIHI ZA KUISHI KATIKA JAMII na ninaamini yale yafunzwayo na maisha tuishiyo mwezi huu, tutayaendeleza maishani
Blogu ya CHANGAMOTO YETU yawatakia wale wote wafungao na kuamini katika mwezi huu, MWEZI NA MFUNGO MWEMA na kwa wale wote waishio na waamini twawatakia ushirikiano mwema kwa waamini
RAMADHAN KAREEM.

Wednesday, July 20, 2011

Enziiiii!!! Tunapoteza nini tunapoongeza nini?

Enzi zangu. Hii ilikuwa ni "one shot" baada ya maandalizi ya kutosha. Hahahahaaaaa. Back in time.
Kwa miongo miwili iliyopita kumekuwa na mabadiliko makubwa saana ya teknolojia. Nakumbuka "enzi" hizo mambo kama kupiga picha ilikuwa ni suala la miadi na mpigaji (kama hukuwa na kamera ndani na naamini wengi hawakuwa nazo), kisha unafanya "zoezi" la style halafu akija unapiga na kusubiri kwa muda (kulingana na ulipo) kabla hujapata picha yako. Nadhani hii ilitufanya tuwe makini saana maana hatukutaka kupoteza picha ama kupiga piucha ambayo tutalazimika kuilipia hata kama hatuitaki.
Lakini sasa kwa teknolojia iliyopo, unaweza kupiga picha 1000 kisha ukachagua moja ya kutumia.
Hivi hatujapoteza kitu kutokana na teknolojia hii? Pengine "za kale" zilitupa maandalizi mazuri katika kujiandaa kupiga picha na mengine mengi ambayo sasa tunayaweka pembeni kwa kuwa tu kuna "teknolojia". Hatutumii ramani tena, tunategemea GPS, hatupiki, ni fast food tuuu. Hatunywi maji yenye usafi wa asili, bali twataka kununua yaliyochujwa toka kwenye maji taka. Hatutembeleani, ni email na jumbe fupi na simu. Hatuaminiani, kila kitu ni kwa "wino wa mashahidi". Hatupendani kwa dhati, mwenye nacho ndiye apendwaye. Yaaani ni mabadiliko kwa kwenda mbele (japo yaturudisha nyuma)Mambo mengi tuyaonayo ya kizamani hunirejesha "back in time" MSIKILIZE INNOCENT GALINOMA HAPA KATIKA WIMBO WAKE ALIOUITA BACK IN TIME

Saturday, July 16, 2011

Tanzanian Student Wins Research Award

Most young people in Tanzania have never heard of the Maryland School of Public Policy. But through the generosity of those who saw the promise in Emmanuel Sulle, he has completed his first year of studies at the School and has also won the Conservation Research in Eastern Africa’s Threatened Ecosystems (CREATE) Research Award from the Frankfurt Zoological Society. Sulle will study the impact of microcredit institutions (in this case Community Conservation Banks) which are in place within the Serengeti ecosystem in Tanzania. Sulle will conduct the field research in Tanzania during the winter break of 2011-2012.

"Emmanuel is a wonderful example of the School's bridge across the oceans--of using the tools of public policy to improve the quality of life and to make a big impact on the world," says MSPP Dean Don Kettl.

Sulle was working as a Research Associate at the Tanzania Natural Resource Forum when he was encouraged by Professor Robert Nelson to apply to the MSPP program. Nelson’s son Fred, who worked 12 years in Tanzania on wildlife conservation, had worked with Sulle on two research studies – most recently the published report on “Biofuels, land access and rural livelihoods in Tanzania”.

“We need more people like Emmanuel,” said Bob Nelson, who also serves as Sulle’s informal mentor. “Unfortunately, they are hard to identify.”

Sulle is currently in Tanzania collaborating with the Maliasili Initiatives to undertake two research projects on “Wildlife Management Areas and Pastoralist Livelihoods: An Assessment,” and “Analysis from Northern Tanzania and Community-based Conservation in the Tarangire-Manyara Corridor: An Assessment of Existing Models and Experiences.”

“Emmanuel is in a position to take his MSPP education and make a serious policy impact in Tanzania,” says MSPP Student Affairs Assistant Director, Taryn Faulkner.

Sulle earned his BA in Economics from St. Augustine University of Tanzania (SAUT) in 2008. He has carried out a variety of research projects commissioned by, or in collaboration with MISERIOR-Germany, Fulbright, Tanzania Natural Resource Forum, Sand County Foundation, and Health and Development International Consultants. He has authored and co-authored a number of research reports on tourism revenue transparency, wildlife management areas, as well as biofuels, land access, and rural livelihoods in Tanzania.

“I am interested to see rational use of natural resources as a tool for poverty reduction in developing countries,” Sulle said.

HONGERA SAANA KAKA SULE. Najua juhudi zako na kwa hakika huu ni uthibitisho wa matunda ya kazi nzuri na ngumu unayoifanya.
Bandio M.T

Nilipokutana na Kaka Emmanuel Sulle, Godwin Meghji, Mobhare Matinyi, Stephen Kasambo na rafiki zao wawili katika jioni ya kumuaga Kaka Steve alipomaliza masomo yake hapa Maryland.

Friday, July 15, 2011

Them, I & Them....ONE TIN SOLDIER...Bushman

TAFAKARI TASWIRA HAPO JUU KABLA HUJASOMA HAPA
Sehemu kubwa ya maisha yetu hutegemea namna tulivyojipanga kuyakabili. Lakini kupanga si rahisi kama hujui undani wa unachotafuta Na ndio maana wapo wanaokosa wanalotafuta kwa kuwa WANAFUATA NJIA ISIYO SAHIHI KATIKA KUTIMIZA MIPANGO YAO.
Nimewahi kuwa na mdahalo na "waamini" wanaoamini kuwa njia ya kubaki mwamini ni kuwatenga na kuwakimbia wasioamini jambo linalonifanya niwaze "Kama Mungu kawapa ukombozi ili wakomboe wasio na ukombozi, ni njia gani wanaoifuata kuusaka ufalme wa mbingu?"
Ninawaona, kuwasoma na kuwasikia wanasiasa wanaoendelea kuamini kuwa VITA ndio njia sahihi ya kusaka amani. Yaani wanajua kuwa kuna AMANI inayohitajika kutafutwa lakini wasilojua ni namna sahihi ya kuifuata amani hiyo.
Labda kwa kuwa ni IJUMAA, turejee kwenye mafunzo yetu ya kimuziki toka kwa wasanii wa Reggae ulimwenguni.
Sina hakika ni wangapi wameshausikia wimbo huu ONE TIN SOLDIER ambao uliimbwa miaka ya 1960 na ambao ni utunzi wao Dennis Lambert na Brian Potter. Kama umeusikia unaweza kuwa umejiuliza maswali mengi kuhusu maana yake. Nimeusikiliza mara kadhaa na kujiuliza kama yaliyoimbwa (ama niseme kutabiriwa) miaka hiyo ndiyo tuyaonayo hivi sasa nchini Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla?
Wimbo unazungumzia watu wa "Mlimani" na "Bondeni" ambao kwa pamoja wanajua kuwa kuna "MALI YA THAMANI" iliyozikwa chini ya jiwe mlimani lakini hawajui ni nini. Na kwa kuwa kuna UROHO wa kutopenda kugawana mali hiyo, wale wa "bondeni" wanapoomba kushiriki katika umiliki wanahakikishiwa hilo lakini wanaishia kuuawa wanapokwenda kuiona kama walivyoahidiwa na wa "mlimani". Na baada ya "kuwafyeka" wale wa bondeni, watu wa mlimani wanakwenda kufunua ilipo mali hiyo ili kujimilikisha na wanakuta HAZINA iliyopo inaomba AMANI DUNIANI. Lakini hiyo ni baada ya kuwa wameshatenda mauaji na kuwateketeza wenzao.
Katika kufananisha nielewavyo mimi na "wachambuzi" wengine, nimekutana na mmoja wa walioelezea maana yake akisema na hapa nanukuu kuwa "greed won't get you anywhere and that betraying your friends will ultimately leave you with nothing but loneliness."
Sijui ni lini wenye imani hawa watatambua kuwa KAZI yao katika wokovu ni kusaidia wengine waokoke? Labda wanaisaka Mbingu kwa kujitenga na kazi itakayowapeleka huko. Labda hawakumbuki masomo ya yule aliyezika talanta.
Pia sijui ni lini viongozi wetu watalitambua hili na kuacha "kuwaangamiza" wananchi wakitaka kujilimbikizia mali zisizodumu? Kuishi maisha ya kifahari ilhali wale waliowapa nafasi walizonzo ili wawatumikie wanahangaika kuiona kesho.
Kaka zangu Kaluse na Kamala wameandika na kuzungumzia saana juu ya hili lakini WATAWALA wetu wameamua kufunga macho na kuziba masikio.
Ukiusikiliza na kuusoma unaelewaje? Fuatilia wimbo huu katika toleo hili lililoimbwa kwenye mapigo ya chant naye Bushman.

"Listen people to a story
that was written long ago,Bout a kingdom on a mountain
and the valley folks below.
On the mountain sit a treasure buried deep beneath the stone
And the valley people thought they'd have it for their very own.

Chorus
Go ahead and hate your neighbor, go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven, you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing On the judgment day
On the bloody morning after one tin soldier rides away.

So the people of the valley sent a message up the hill
Asking for the buried treasure tons of gold for which they'd kill
Came an answer from the mountain,
"with our brothers we will share, All the secrets of our mountain,
all the riches buried there."

Now the mountain cried with anger,
"Mount your horses, draw your swords"
And they killed the valley people, so they won their just rewards
Now they stood beside the treasure on the mountain, dark and red
Turned the stone and looked beneath it, "Peace on earth" that all it said.

Chorus
Go ahead and hate your neighbor, go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven, you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing On the judgment day
On the bloody morning after one tin soldier rides away.".... x2


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.IJUMAA NJEMA

Tuesday, July 12, 2011

Tanzania Yangu.....Iliyo "bize" kumwagilia matawi badala ya mizizi (II)


Novemba 27, 2009 niliandika sehemu ya kwanza ya bandio lenye kichwa kama hiki. Japo si katika maudhui yanayofanana kabisa, lakini naamini bado kichwa hiki kinafaa hapa. Na pia nikumbushe kwamba Februari 2, 2010 niliandika kuhusu WAKUU WA MIKOA nikiuliza kama ni watumishi wa wananchi ama ni mzigo kwa serikali na wananchi? Pia nikaeleza niaminivyo kuwa ni CHANZO CHA KUDIDIMIA MAENDELEO MIKOANI
Na leo ningependa kuiangalia mikoa yenyewe.
Maendeleo yake na namna yapatikanavyo. Na mengine mengi
Nimekuwa nikiwaza kuwa MIKOA ina mahitaji mbalimbali na inahitaji pesa kuyatimiza.
Ni vipi inapata pesa zake? Na wapi inapopata?
Katika "bandiko" langu kuhusu WAKUU WA MIKOA, nilisema "NALOAMINI NI KUWA, Endapo wakuu wa mikoa wangekuwa wanagombea basi wangekuwa na ubunifu wa kutumia rasilimali zilizopo mikoani ili kukamilisha bajeti na mahitaji ya mikoa wanayoiongoza na kupunguza kutegemea ruzuku za serikali kuu. Mikoa yetu ina rasilimali nyiiingi na kama ingetakiwa kujiendesha kwa kujitegemea nina imani kungekuwa na ubunifu na uchungu wa kutumia rasilimali hizo. Lakini kwa sasa sioni kazi za wakuu wa mikoa kwa sababu ndani ya miaka mitano ya Rais, wengine wanakuwa wameshahama "vituo" vya kazi zaidi ya mara mbili na hakuna la maana wanalofanya kuiendeleza. Naamini ni mzigo kwa serikali na wananchi kwa ujumla."
Bado naamini hivi. Sijawahi kusikia BAJETI YA MKOA fulani na kama ipo sina hakika kama hutofautishwa kulingana na mahitaji. Yawezekana Dar Es Salaam ikawa na bajeti kubwa ya ulinzi (kutokana na wageni wanaoitembelea) kuliko Rukwa, lakini ni nani ajuaye? Ni kipi chanzo cha mapato cha mikoa hii na ni nani anayepanga bajeti yake? Ni yupi anayetoa uwiano wa kiasi gani kiende wapi ikiwa fedha za KUENDESHA MIKOA zinatoka serikali kuu? Na kama ndivyo, ni kweli kuwa Mbeya (waliomrushia Rais mawe) watapata fursa sawa ya kipato sawa na Pwani? Na je, mikoa kama Arusha ambao wana rasilimali nyingi ambazo wangeweza kuzitumia kupata kipato cha mkoa na kuendeleza shughuli zao, watapata fungu sawa licha ya kuwa na wapinzani wengi bungeni?
Ni kweli kuwa mikoa kama Arusha ama Shinyanga na hata Mara inastahili kuwa na shida kwenye shule zao kama mikoa mingine? Naamini kama wangekuwa na bajeti zao, na kutenga fungu kutokana na makusanyo yao, na kugawa makusanyo kulingana na mahitaji yao, basi shule katika baadhi ya mikoa zingekuwa bora, barabara zisingefanana na mishahara ya baadhi ya wafanyakazi wa ngazi za mikoa isingechelewa.
Ni kweli kuwa tunaweza kujenga serikali kuu bila kujenga ngazi za chini?
Ni kweli tutaweza kudhibiti na kuwa wazi katika bajeti ya serikali kuu kama hatujui ya mkoa?
Wananchi wana nguvu ama maamuzi gani kuhusu bajeti ya mikoa yao?
Matumizi yake je? WANASHIRIKISHWA?
Katika Hotuba ya Mwaka Mpya 2011 ya Rais Jakaya M. Kikwete, aligusia kile alichokiita NIDHAMU YA MATUMIZI ambapo alisema (na hapa namnukuu) "Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa nidhamu ya matumizi bado hatujapiga hatua ya kunifanya nipoe moyo, ingawaje kuna mafanikio yanayoendelea kupatikana. Niliwakumbusha Mawaziri kuhusu kuwepo Kamati za Matumizi ya Fedha katika kila Wizara, Idara za Serikali na Halmashauri za Wilaya na Miji ambazo niliagiza ziundwe miaka mitatu iliyopita.

Niliwakumbusha kuwa, wakuu wa taasisi hizo ndio wanaoongoza Kamati hizo na hivyo wao ndiyo wanaoongoza Kamati za Wizara zao. Nimewataka wahakikishe kuwa Kamati hizo zinatekeleza ipasavyo majukumu yake ili rasilimali za taifa zifanye kazi iliyokusudiwa. Halikadhalika, niliwataka wahakikishe kuwa Kamati za Idara na Mashirika chini ya Wizara zao zinafanya kazi kwa ukamilifu.

Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa Halmashauri za Wilaya na Miji, mwaka huu tuliendelea kuziimarisha Idara za Uhasibu na Ukaguzi wa Ndani. Tutaendelea kuhakikisha kuwa kila Halmashauri ina Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani wenye ujuzi na sifa zinazostahili za kitaaluma, uaminifu na uadilifu."


Kama tunataka kujenga serikali kuu iliyo na NIDHAMU YA MATUMIZI, ni lazima kuwa na NIDHAMU YA MATUMIZI katika ngazi zote za utawala.
Lazima tujue kuwa wengi wa wafanyakazi / watawala walio serikali kuu wametoka ngazi za chini. Na bila kuwaengea UAMINIFU NA UADILIFU katika hatua za awali, tusitegemee kuwa na serikali kuu yenye UADILIFU.
Ni wakati wa kujua kuwa licha ya kwamba matokeo ya utendaji m'bovu yanaonekana kama maamuzi ya serikali kuu, lazima tujue kuwa kurekebisha hilo kwahitaji ngfazi za chinbi. Kama ambavyo tunaona majani yakikauka tukamwagilia mizizi.
TUONANE "Next Ijayo"

Sunday, July 10, 2011

Milionea...... bado anakusanya taka....ANAWAZA NINI?

Photo Credits: Dailymail.co.uk
UKISHINDA MILIONI KADHAA (tena namaanisha dola milioni kadhaa) UTABADILI VIPI MAISHA YAKO?
Nakumbuka mwaka 2000 nilikuwa nikiongea na Kaka yangu Lwaga Anangisye na katika maongezi akazungumza suala la NDOTO. Yeye aliliweka kwenye "lugha ya msisitizo" aliposema DREAMS. Kisha akasema neno ambalo mpaka leo likingali akilini mwangu. Kwamba "watu wengi wanaishia kutofanikiwa hata wanapopata nafasi kwa kuwa wanakuwa hawajajiandaa." Akasema kuwa wengi wetu hatuangalii lolote lililo zaidi ya uwezo wa sasa. Kisha akaniuliza, "ukipewa milioni moja sasa hivi ufanyie jambo la maana, utafanya nini?" Hilo pekee lilikuwa SWALI TOSHA KUNIAMSHA.
Nimekumbuka hilo baada ya kusoma kuhusu Bw Tyrone Curry. Mwanaume ambaye alishinda dola milioni 3.4 lakini bado anaendelea na kazi yake ya kusafisha vyoo na kukusanya takataka
Mzoa taka huyu ambaye aliwahi kuwa mwalimu, sasa ana kazi ya pili shuleni hapo ambayo ni kocha. Na kati ya zawadi alizotoa kwa shule "anayoitumikia" ni kuinunulia timu yake gari jipya lenye thamani ya dola 40,00.
Suala hapa ni kwamba licha ya kushinda dola milioni 3 na zaidi, Tyrone alipoulizwa kwanini anaendelea kufanya kazi anasema "You need to be doing stuff: That’s my philosophy.” Anapoulizwa kwanini anaendelea kuishi katika nyumba ya awali na hajabadilika, anasema "My mom was the mother of the neighborhood. All the kids came to our house, so that’s why my home is open, too. People come, they eat, and they have fun. Before I won the money, I struggled. Sometimes I fell behind, but I always remember my mom’s words: ‘You can have somethin’, but that person next to you might not have anything. If you look out for that someone, they’ll look out for you.’" na kisha kuhusu maisha yao (kama familia) anasema hayabadilika na "We don't even go out to dinner. We cook at home.”
Na ndio maana nikaanza kwa swali nililoanza nalo. ALIWAZA / ANAWAZA NINI KUFANYA KAZI LICHA YA UTAJIRI ALIONAO?
Tazama video inayomhusu hapa chini.



***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

Thursday, July 7, 2011

Si tatizo iwapo utaliangalia toka "pembe nyingine"

Wengi wenu mmeshuhudia UKIMYA niliokuwa nao mtanmdaoni. Tatizo kubwa lilikuwa ni MTANDAO. Na kwa juma zima nikahangaika na "provider" wangu kuweza kunirekebishia tatizo bila mafanikio.
Alipofanikiwa kurekebisha tatizo, akasema "kutokana na siku ambazo hukuwa na huduma, hatutakulipisha gharama kwa wiki nzima. Hivyo ankara yako ijayo itapunguzwa dola 21".
Fikra za awali zilikuwa ni kughafilika kwani niliwaza huyu "huyu mtu hajui ni kiasi gani nimeshindwa kuwasiliana na watu wangu, na anadhani thamani yake ni dola 21?"
Lakini muda mfupi baadae nikaliangalia "tatizo" toka pembe tofauti na nikagundua kuwa wamegawanya ankara yangu ya mwezi kwa siku nilizokaa bila huduma wakapata gharama hiyo, hivyo ndio gharama halisi.
Na badala ya KUKASIRIKA KUWA WANANIREJESHEA DOLA 21, ni vema nikafarijika kuwa NINALIPA DOLA 21 KWA JUMA ZIMA.

NILILOJIFUNZA ni kuwa badala ya kukasirika kuwa nimepunguziwa kiasi kidogo cha dola 21, ninaweza kumshukuru Mungu kuwa gharama ya mawasiliano ya simu na internet kwa siku zote nilizokosa ni dola 21. Hii ilinifanya nione kuwa si tatizo. Sio kwa sababu lilitatuliwa, bali kwa kuwa nililiangalia kutoka PEMBE NYINGINE. Na hilo limenifanya nitambue kuwa katika mengi tuonayo, yawezekana SI TATIZO IWAPO TUTAYAANGALIA TOKA "PEMBE NYINGINE"