Saturday, October 8, 2011

Mahojiano na Upendo Nkone, Upendo Kilahiro na Christina Shusho.

Shukrani za pekee kwa waimbaji hawa ambao waliweza kutoa muda wao wa mapumziko (ambao wangeweza kufanya lolote watakalo) kuweza kuzungumza machache kuhusu HUDUMA wanayoitoa. Wameeleza historia zao kwa ufupi, kufafanua kile wafanyacho (kama ni huduma, kazi, usanii, hobby ama ni vipi?), hujuma zinazofanywa katika soko na biashara ya muziki nchini, namna wanavyotunga nyimbo zao, tofauti ya INJILI ya Tanzania na nchi walizotembelea pamoja kile / vile walivyojifunza katika ziara yao ya hapa Marekani ambacho wanaamini hawatakisahau.
KARIBU

Thanks and Praises ni kipengele kinachozungumzia masuala ya imani na kurejesha SIFA NA SHUKRANI KWA Muumba. Kwa matoleo zaidi ya kipengele hiki, BOFYA HAPA
Photo Credits: Vijimambo

10 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Video imegoma, nini, Mkuu? Mbona mie hapa sipati? Au niko bondeni mno?

Mzee wa Changamoto said...

Heshima kwako Kaka Goodman.
Pole kwa hilo. Niligundua makosa kiasi nikaamua kuivuta kando kurekebisha. Sasa ipo na naamini utaweza kuipata vema
Baraka kwako na KARIBU

Yasinta Ngonyani said...

Umefanya kazi nzuri...ahsante sana

Rachel Siwa said...

Hongera kaka, Kazi nzuri na yakuvutia, Ubarikiwe na Ahsante.

tanzaniakwetu said...

Kazi nzuri sana bro!
Ukiwa unahitaji kupata link mbalimbali za kitanzania tembelea www.tanzaniakwetu.com
kila aina za link zipo, za dini na nyinginezo!
Karibu!

Simon Kitururu said...

Kazi mwanana!

(MMN) said...

Safi sana. Ni waimbaji wenye vipaji sana. Mungu Aendelee kuwabariki!

Goodman Manyanya Phiri said...

Nashukuru kupata ujumbe wa marekebisho, Mkuu; nitarudia kuwasikiliza wanadada wale. Kwani muziki wao nimeugundua miaka miwili iliepita nikiwa natembelea Tanzania kutoka Afrika Kusini. Nilibarikiwa na kuburdudishwa sana na sauti zao!

Godwin Habib Meghji said...

Kazi nzuri sana..

Unknown said...

Great I watched it on YouTube and these are wonderful women.God's creation which is magnificent in a particular sophisticated unique way...we are of no match with God's beautiful Angel and they are our beloved blessing...be blessed too.Love you...Shusho ,Upendo,+the other Upendo love you...love you