Thursday, April 19, 2012
Pongezi na shukrani toka ubalozini
Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya Wenzangu hapa Ubalozini napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Watanzania wote walioshiriki kwa wingi katika Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washington Metropolitan. Nimefurahishwa sana na moyo wa Umoja na Ushirikiano ulioonyeshwa na Watanzania wote waliojitokeza katika mkutano huo wa Uchaguzi.
Aidha napenda pia kutoa shukurani zangu za dhati kwa Kamati ya Mpito, chini ya Mwenyekiti wake Givens Kasyanju kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuandika Katiba mpya, kuandaa na hatimaye kusimamia kufanyika kwa Uchaguzi huu wa kihistoria wa Jumuiya ya Watanzania DMV. Asanteni sana.
Mwisho napenda kuwapongeza kwa moyo wa dhati Viongozi Wapya waliochaguliwa kuiongoza Jumuiya ya Watanzania DMV. Napenda kuwahakikishia ushirikiano usio na mipaka kutoka kwangu binafsi na kwa wenzangu hapa Ubalozini katika kufanikisha kila lililojema kwa manufaa ya Watanzania wote waishio DMV.
Mheshimiwa Mwanaidi Sinare Maajar
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico
Washington, DC.
April 16, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment