Wanawake wasomi na wenye ushawishi nchini Tanzania wameaswa kushauriana na wanawake wenzao kama njia ya kukomboana katika maisha.
Balozi wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali, aliyasema hayo katika mahojiano maalum aliyofanya nasi (pamoja na mwenzangu Abou Shatry wa blog ya Swahilivilla) ambayo yalirushwa na kituo cha redio cha Ebony FM ya Iringa kwenye kipengele chake cha Red Carpet kinachozungumzia masuala ya wanawake.Katika mahojiano haya, Mhe Wazir anazungumzia mambo mbalimbali yahusuyo wanawake kama vile mwamko wa mwanamke katika elimu, nafasi ya mwanamke kwenye nafasi za uongozi, changamoto za kuwa mwanamke na balozi, nafasi ya mwanamke katika maamuzi, jambo lililomfurahisha na lile lilimsikitisha na mwisho ushauri wake na wananchi.
Katibu uungane nasi hapa kwa mahojiano kamili
No comments:
Post a Comment