Wednesday, July 18, 2012

SHUKRANI

 
Tunapenda kuleta shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshiriki katika kuuguza na kasha kusafirisha mwili wa ndugu yetu Domitian Rutakyamirwa nyumbani Tanzania kwa mazishi.

Mwili ulisafiri salama na mazishi yalifanyika Jumanne ya tarehe 3 mwezi huu na mkewe kurejea hapa Marekani mwishoni mwa wiki iliyopita 

Shukrani za pekee kwa Madaktari na wauguzi wa Hospitali za Chuo Kikuu cha Howard na Chuo Kikuu cha George Washington, Viongozi wa Dini waliomhudumia katika siku zake za mwisho, kwa Kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries na washarika wake kwa kufanikisha ibada ya kumuaga ndugu yetu mpendwa, kwa Rais, Katibu na Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia, kwa ndugu, jamaa na marafiki wa mbali na karibu ambao walijitokeza kumhudumia alipokuwa amelazwa na hata kusaidia familia kwa ushauri, hali na mali katika wakati mgumu waliokuwa wakipitia. 

Tunaamini kuwa UPENDO mliouonyesha kwetu utaendelea kwa wengine kwani katika nyakati kama hizi, ni UPENDO pekee ulio nguzo kuu kwetu. 
Mungu awabariki katika kila jema mfanyalo. 

Asanteni 
Kamati ya Msiba

2 comments:

emuthree said...

Jinsi unavyoliangalia ni tatizo pia!

Mungu awape subira nyote, na yote ni mapenzi ya mungu!

Yasinta Ngonyani said...

Kuwa na ushirikiano wa aina hii wakati mpo ugenini kwa kweli inatakiwa..kuwa na UMOJA sio kwa KUBWA tu hata DOGO...Mungu awabari wote.