Sunday, July 1, 2012

Ya Dr. Ulimbomba na akisi UTU wetu.

Kati ya habari za kusikitisha hivi karibuni nchini Tanzania ni kitendo CHA KIBINADAMU (kwa kuwa hakuna mnyama anayejulikana kutenda haya) alichofanyiwa Kiongozi wa mgomo wa madaktari nchini Dr. Ulimboka David.
Daktari huyu ambaye kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa ALITEKWA NA KUTESWA sana ikiwa ni pamoja na kung'olewa baadhi ya kucha na meno, amesafirishwa kwenda nje kwa matubabu zaidi.
Lakini NINI CHANZO CHA HAYA YOTE?.......UTU. 
UTU wa wale waliosababisha mgomo huu kuanza. Wapo wanaolaumu serikali kwa kupuuza UTU wa madaktari na kutotimiza mambo ambayo walikubaliana.
Lakini wapo wanaolaumu UTU wa madaktari kwa kuendekeza maslahi yao mbele na kusahau umuhimu wa kazi zao na hata maisha ya wananchi wasio na hatia wanaopoteza maisha yao.
Wapo wanaolaumu UTU wa wale waliomteka mtu aliyekuwa akitetea UTU wa madaktari ambao wanaonekana kutojaliwa na hivyo kuathiri UTU wa watu wengi nchini.
SINA HAKIKA na chanzo halisi cha tatizo, na siamini kama ni madaktari ama wafanya maamuzi serikalini wanaoathirika na mgomo huu, lakini ninalojua ni kuwa UTU umewekwa kando katika tatizo hili.
Tumekosa UTU kwenye sababu mpaka namna ya kupata suluhisho la tatizo hili.
Kilichomkuta Dr Ulimboka, ni hakika UKOSEFU WA UTU na kutanguliza maslahi binafsi ambayo sio tu yanadhihirisha ukatili wa binadamu, bali pia yanazidisha ukatili kwa binadamu.
Tumeona kuwa hata idadi ya madaktari waliogoma imeongezeka katika kukerwa na kilichomkuta mwenzao ikimaanisha kuwa hata waathirika wa mgomo wameongezeka. UTU WA WENGI ZAIDI UKO MASHAKANI.
YAMEANZIA WAPI?...NA MWISHO WAKE NI UPI?
Labda maswali haya yafuatiwe na swali la NI NANI MUATHIRIKA wa mgomo huu?
Yote juu ya yote, iwapo tungeweka UTU mbele, maombi ya madaktari yangeangaliwa vema, na madaktari nao wangedai kwa UTU zaidi na hivyo UTU wa wananchi sisi usingekuwa hatarini.
Hata wale waliodhani kutatua mgomo kwa kutenda yasiyo na UTU kwa daktari huyu wangetumia njia nyingne, tungekuwa na MTAZAMO MWINGINE kuhusu tatizo hiliu.
TUREJESHE UTU katika kutafuta suluhisho la matatizo yetu, kwani kukosekana UTU kunaathiri zaidi UTU wa wale walio mbali na mgogoro husika.

2 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by the author.
emuthree said...

Utu ukishaondoka kwa binadamu, ubinadamu unaondoka na unyama hushika nafasi,na hapo binadamu anafanya yale anayoona yanamfaa bila kujali athari zake kwa wengine.

Mkuu pole sana kwa majukumu, tupo pamoja

Monday, 02 July, 2012