"HALI YA UCHUMI WA DUNIA NI MBAYA"
Kauli hii tumeisikia mara kwa mara na imekuwa ikitumika zaidi ya UHALISIA wake. Ni kauli ambayo inatumika kuwatisha wananchi na pia kutumiwa na WATAWALA KUKWEPA MAJUKUMU YAO.
Hivi sasa kila kitu kisichokamilika chaonekana kuwa na sababu hii ya "mvurugiko wa uchumi". Hata wabunge hawatembelei majimbo ya (japo wanapaswa kuishi huko) sababu hii
- Wananchi hawapati maendeleo sababu ya mvurugano wa uchumi.
- Sera za serikali ya awamu ya nne hazikamiliki kwa sababu hiyohiyo
- Sitashangaa nikisikia kiongozi akisema WANAKULA RUSHWA SABABU HIYO.
Ukweli ni kwamba WANASIASA hawana mipango endelevu na sasa wanatumia hili la uchumi kuharibika kama kisingizio. Ni kweli kuwa kuna mambo yaliyokwamishwa na mvurugano wa uchumi, lakini bado kuna mengi tunayoweza kufanya kwa NGUVUKAZI na kuwezesha kuibadili jamii.
Kujenga zahanati, Kuchimba mitaro, Kuchimba visima, Kutokomeza Rushwa, Kuchonga / kutengeneza madawati na mengine kama haya ni baadhi ya mambo yanayohitaji nguvukazi na ushirikiano kati ya WATAWALA na wananchi.
HUU SI WAKATI WA KUTISHANA. NI WAKATI WA KUELEZANA MAJUKUMU YETU NA KUPANGA NAMNA YA KUYAKABILI. Na kwa kuyakabili kwa umoja (licha ya ugumu wake) tutafanikiwa na kujivunia. Hizi ni nyakati ambazo wanasiasa wanapaswa kuwaeleza wananchi kuwa HALI YA UCHUMI ISEMWAYO SI MWISHO WA DUNIA na kisha kuwaonesha mahala pa kwenda kutua mzigo wao wa msongo wa mawazo (stress)
Sijui ni kwanini kila wazungumziapo KUONDOA STRESS wanahusisha na mto, lakini ukweli ni kuwa KILA MTU ANA "MTO" WAKE ANAOWEZA KWENDA NA KUTUA MZIGO WAKE NA KUANZA UPYA MAISHA MAPYA, MAISHA CHANYA NA KUFANIKIWA.
Tuachane na siasa, tugeukie kwenye kipengele chetu cha kila mwisho wa juma ambapo huwa tunahusisha WIMBO WA REGGAE na maisha yetu ya kila siku.
Na leo, tunaendeleza desturi yetu hiyo kwa kuangalia namna ambavyo msanii chagu letu hii leo amehusisha MAISHA MAGUMU na PUMZIKO tunalohitaji ili kusonga mbele. Anazungumzia HITAJI LA IMANI KWA MUNGU ambaye ndiye muweza yote.
Namzungumzia Nasio Fontaine ambaye anazungumzia kuhusu kutambua ulipo "mto" wako kisha kuelekea huko "kutua mzigo wako" kisha kuanza maisha mapya. Anasema anajua MUNGU NDIYE SULUHISHO PEKEE HATA KAMA UNAHISI KILA KITU HAKIENDI VEMA KWAKO.
Msome na kumsikiliza katika wimbo huu NEW SONG
Yeah!, we really wanna say now.
Come down to the river, lay down your burdens,
walk away and singing a New Song, sing a Brand New Song
Come to Mount Zion Jah Seh, lay down your burden
Walk away and singing a New Song
Sing a brand new song
I know your burdens feels so heavy,
you feel you couldn't carry no more,
yet here comes another hurdle,
higher than the one before,
and i know the road you trod,
is rough and rugged,
still i know,
the Lion of the Judah is the only solution"
Come down to the river, lay down your burdens,
walk away and singing a New Song, sing a Brand New Song
Come to Mount Zion you heavy laiden, lay down your burden
cause you've been burden for much too long
Journey is tough, the road is steep
And there's no rest for weary feet.
Yet here come another stumbling block
Greater than the one before
And i know that you've been through
Soo Much, Too Much
And HARDER THE BATTLE, TOUGHER THE FIGHT
SWEETER THE VICTORY
Come down to the river, lay down your burdens,
walk away and singing a New Song, sing a Brand New Song
Come to Mount Zion Jah Seh, lay down your burden
cause you've been burden for much too long
For much too long
Come, come, come come, come to mount Zion
Lay down your burden
Cause in my Father's House
There is many a Mansion
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
No comments:
Post a Comment