Saturday, January 5, 2013

Happy Birthday Dad

Baba na wanawe wa kiume. Lol
 Leo ni siku muhimu saana familiani mwetu kwani NGUZO MUHIMU katika familia inazidi kuimarika. Ni siku ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baba yetu mpendwa. Naamini nilishaeleza namna ambavyo Babangu amekuwa amekuwa na VYEO zaidi ya UZAZI kwangu.
Alianza yeye kunishika hospitali
Nami nikamshika Paulina miongo kadhaa mbele
Kisha nikabarikiwa "kumkamata" Annalisa
Na ninavyozidi kukua na kuchukua majukumu ya uzazi, nazidi kutambua uwezo mkubwa wa fikra na upendo aliokuwa nao na ambao anaendelea kuwa nao kwetu. Najifunza kuwa kuna mengi ambayo niliyachukulia kimzaha na sasa natazama nyuma na kuona namna ambavyo TUMEBARIKIWA KUWA NA BABA KAMA YEYE.
Baba, wakati unasherehekea siku yako ya kuzaliwa, napenda utambue kuwa ULIWEKEZA MEEENGI MEMA KWETU na sasa tunaendelea kuvuna.
Tunajifunza kutokana na maisha uliyotufunza na tunaendelea kuwafunza wengine. Kuwa na Baba kama wewe ni faraja na hakuna siku nitawaza kuwa na baba tofauti nawe.
TWAKUPENDA na TWAKUOMBEA
Happy Birthdate Dad

Dadangu Yasinya wa Blogu ya MAISHA naye anakumbuka siku yake ya kuzaliwa na sina ninaloweza kukuombea zaidi ya MAISHA MEMA NA MAFANIKIO
Happy Birthadate Da Yasinta
Naye Kaka Haki Ngowi wa blogu ya Blogu ya Food For Thought anatimiza miaka kadhaa siku ya leo. Huyu ni kati ya watu wa mwanzo ku-post mabandiko yangu kwao kabla hawajanishauri kufungua kibaraza changu hiki cha Changamoto Yetu. Heshima kwako Kaka na nakutakia mafanikio na kila lililo jema.  
Happy Birthday Kaka Haki
HAPPY BIRTHDATE TO YOU ALL

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Ni HESHIMA KUBWA SANA KUWEKWA HAPA KATIKA HII BLOG YA CHANGAMOTO NA KUTAKIWA KILA LA KHERI KWA SIKU YA KUZALIWA..Nami napenda kuseam hongera sana kwa wenzangu kama baba hapo juu na kaka Ngowi kwa siku yetu.