Familia ya Ngireu inawataarifu ndugu, jamaa na marafiki kuwa misa
na kumuaga marehemu Marehemu Martin Ngireu (pichani juu) itafanyika kesho Jumamosi May 25, 2013 kuanzia saa 6 mchana
mpaka saa 10 jioni (12-4pm)
Misa hiyo itafanyika
313 Talbot Avenue,
Laurel, MD. 20707
Baada ya misa, kutakuwa na kutakua na chakula kwenye address 210 Patuxent Road,
Laurel MD 20707
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu inafanywa.
Kama ilivyodesturi yetu kupeana pole ndio ustaarabu
wetu. Msiba upo 210 Patuxent Road, Laurel MD 20707.
Tafadhali tenga muda wako kufike na kuwapa pole watoto wa
marehemu Carol na dada yake waliokuja kutoka Tanzania na California.
Msiba huu ni wetu sote DMV tafadhali tujumuike na tuwafiriji wafiwa.
Kushirikiana na kushikamana kwa shida na raha ndio staili na maisha yetu
DMV.
Kwa maelezo na maelekezo tafadhali wasiliana na Mtoto wa Marehemu Carol 301 957 4523.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.
No comments:
Post a Comment