Monday, July 15, 2013

Porojo za Mjinga mie na "MJOMBA"

Sh'kamoo Uncle.
Yaani wikiendi ilivyoenda haraka, hata huwezi kuamini kuwa ni yaleyale masaa 48 tuliyokuwa tukipata enzi za kuwategemea wazazi.
Lakini ndio ukubwa.
Halafuuu...
Nimegundua kuwa kama mtu hajafanya kitu, basi hata hajui ugumu wake na wakati mwingine anashindwa hata ku"aprishieti"mambo.
Mimi sasa hivi na"aprishieti" malezi ya wazazi wangu kuliko zamani. Nadhani kwa kuwa na mimi sasa ni mzazi kwa hiyo naona walivyo"strago" kutulea.
Hilo ndio limenifanya nihisi hata u-Rais ni kazi kuliko tunavyodhani.
Hivi Anko.......
Kulingana na ugumu wa kuwa Rais, umeshafikiria kuONGEZA idadi ya wasaidizi kwenye mambo mengine ambayo nahisi huyawezi peke yako?
Mfano...
Kuwa na MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU.
Maana mimi hata ahadi ulizotoa kwenye kampeni ya 2010 pale Bukoba sizikumbuki zote, itakuwa za nchi nzima?.
Hapo achilia mbali zile za 2005
Nadhani kungekuwa na mtu wa kukukumbusha kuwa "Uncle 'ake Mube, bado hujajenga hata choo kipya tangu utembee Magereza 2006?" nk.
Yaani....
Kukumbusha tu mambo kibao.
Hao wasaidizi ulionao sijui wanakuogopa?
Wamekwambia kuhusu "KILIO" cha watu walio jela kwa kubambikizwa kesi?
Achilia hawa kina Babu Seya ambao hawakufanyiwa DNA wakati wao na washukiwa wa kulawitiwa walikuwepo, na watu bado "wanachoooonga", kuna wale WATOTO inaosemekana "wanachomewa" na mabosi wao.
Mie nakukumbusha ile hali ya magerezani.
Ukipata nafasi, watembelee tena maana niliskia Da Kajala akitoa wito kwenu kusaidia kule maana WAPO WENGI WASIOSTAHILI KUWEMO MLE NA AMBAO KODI INAWALISHA KIMAKOSA ILHALI WAHALIFU HAWANA PA KWENDA.
Ukiwa na mtu wa kukukumbusha haya, akahimiza kuhusu HAKI YA WAFUNGWA, kisha ukahahakikisha WANAOFUNGWA NI WAHALIFU, basi nina hakika tutakuwa tumetimiza lengo la magereza kuwa CHUO CHA MAFUNZO na sio STORAGE YA WANAOCHUKIWA NA WENYE NAZO.
Anyway Anko.
Wacha nirejee mtaani waliko wenzangu. Nikipata nafasi ntakusimulia wanayosema kesho

No comments: