Monday, September 2, 2013

Mahojiano na Mike Mhagama......BONGO FLAVA.

 Mike Mhagama (L) "enzi" zake akiwa studio za Radio One Stereo. Kulia ni Mike wa Sasa
Picha kwa hisani ya ukurasa wa Facebook wa Mike Mhagama
Michael Pesambili Mhagama ni mmoja wa watangazaji wa awali waliojikita katika harakati za kuutambua, kuuboresha na kuupa hadhi muziki ambao sasa unatambulika kama BONGO FLAVA.
Pia ndiye aliyeanzisha JINA hilo la Bongo Flava alipokuwa Radio One Stereo.
Kikosi kamili kilichofanya vema zaidi Radio One. Yeye (Mike Mhagama) alikiita "The Dream Team aka The Academy!"
Jumamosi ya Aug 31, 2013, alifanya mahojiano na JAMII PRODUCTION na kueleza mengi kuhusu Muziki huu wa Bongo Flava
Ameeleza harakati zao kuuweka kwenye ramani ya muziki nchini, matatizo yanayoukabili, mafanikio na hata ambapo angependa kuuuona ukifika na kuwafikisha wahusika wake.
Unajua jina BONGO FLAVA lilipotoka na lilivyotokea?
Alikabiliana vipi na UTATA WA MUASISI WA JINA BONGO FLAVA? Lakini je! Ni yeye muasisi wa harakati za kuwa na muziki huu radioni?
Anauonaje muziki huu? Unakua ama?
Wito kwa wasanii na wadau wote wa muziki huu nchini ni upi?
Karibu uungane nasi
NB: Tunaomba radhi kwa ubora wa sauti katika sehemu za mahojiano haya

1 comment:

Egidio Ndabagoye said...

Kama unapata pesa kwenye kazi yako...invest kwenye kazi yako...hiyo ndio kazi unayofanya...inayokupa pesa.--Mike Mhagama

Safi sana kaka Mubelwa