Monday, November 17, 2008

HAPPY BIRTHDAY MAMA


" We each get just one MOTHER to love a lifetime through, One MOTHER to encourage us in everything we do. But one MOTHER is so many People blended into one. A source of inspiration and happiness and fun. A MOTHER hears out every word. She listens with her heart, shares and always cares, thinks of others first and she'll love us just like always even when we're at our worst. She brings such happiness with kindness she gives and creates a GOOD EXAMPLE simply with the life she lives. YES! We only have ONE MOTHER to look up to and to praise and NO ONE ELSE IN ALL THE WORLD can MATCH HER LOVING WAYS"

Namna siku zinavyokwenda ndivyo tunavyozidi kuangalia nyuma na kutambua umuhimu wa yale yote mliyokuwa mkitufundisha. Tunayatambua kwa kuwa yanatusaidia sana maishani popote tulipo ambako ni mbali nanyi.
Ni malezi ambayo mlitupatia katika muda wote tuliokuwa chini ya uangalizi wenu ambayo yanatuwezesha kuishi popote tuendapo na ni msingi wa Heshima na Upendo pamoja na Imani mliyotujengea ambayo inatuongoza vema wakati wote.

Tangu siku hii ya kwanza uliponitwaa mikononi mwako mpaka siku hii tunayopishana kidogo kimo, bado waendelea kuwa Mama yuleyule mwenye upendo usiopimika.
Mama; waweza kutokuwa maarufu kama wengine, kutoonekana na kusikika kama wengine, lakini utambue kuwa hata katika usiri wa maisha yako, wewe bado ni SHUJAA wa maisha yetu na wale wote tuhusianao nao na kwa hakika TUNAJIVUNIA wewe kuwa MAMA yetu. Tunakupenda na kukuthamini na tunakutakia kila la kheri katika kukumbuka siku yako ya kuzaliwa na pia katika miaka ijayo yenye afya na nguvu tele.

HAPPY BIRTHDAY MAMA
Na huu ni wimbo kwa Mama, toka kwao Boys II Men . Blessings

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa hakuna kitu/mtu ambaye anaweza kufananishwa na mama. kwani ni mmoja tu

Mzee wa Changamoto said...

Thanx Yasinta. Kuna wakati ambao uhusiano wa Mama na mwana unakuwa very very personal na ni kutokana na majukumu ya asili wanayokuwa nayo kinamama kwa watoto wao.
Nasi ni vivyo hivyo.
Blessings

MARKUS MPANGALA said...

HODI HODI HODI HUMU NDANI.
ndiyo mambo ya raha haya kublogu.
Asante mzee wa changamoto, kwani mama ni mama hata kama hana macho,masikio,meno,pua n.k {huu ni mfano}. haya kazi njema kaka
wape salamu wote waambie KARIBU SANA NYASA.

Subi Nukta said...

Naona unajidai sana! Na kwa kweli haki ya kujidai unayo! Ringa kijana, tembea kifua mbele, kwani NANI KAMA MAMA? (hata baba si sawa na Mama kwa kuwa baba ana heshima yake ya kipekee kwa vile hata yeye NANI KAMA BABA?).
Hongera kwa sikukuu ya Mama.

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto, kweli ni changamoto. Nimesoma mashairi uliyomtumia mama yako, akija toka Dodoma nitamfungulia blog hii asome kwa wakati wake. Baba yako amefurahia sana nasi tunadhani kuwa tunahitaji kujivuna kwa kutambua mchango wa wazazi wako. Mungu azidi kukupa busara hii na uendelee na maisha ya tafakari njema. UBARIKIWE

Euniace

Anonymous said...

Anonymous
Mama yako ameyaona mashairi na amefurahi sana na kuema kuwa anajisikia na kujivunia kuwa na watoto wanaoweza kutambua mchango wa wazazi wao maishani mwao. Hata hivyo mama na baba na mama mdogo na baba mdogo walijisikia kutaka kusema kidogo kuhusu jina kama ulivyoeleza kwenye blog ya wakati huu. Ni kweli kuwa ni vigumu kumwambia mtoto maana ya jina pale unapompa lakini ni kweli pia kuwa mtoto akipata ufahamu anaweza ama kujisikia vema au vibaya kutokana na jina alilopewa na wazazi, hii huwalazimisha wazazi kutafakari maana kabla ya kutoa jina. Maana hata kama jina laonekana kuwa limepinda au la kimizengwe, huwa kuna sababu za jina hilo na wazazi wakiulizwa maana wanaweza kusema.
Ni vema kuchagua kwa makini jina la mtoto, maana katika kutoa jina si vema kuangalia mambo ya karibu sana na yanayopita, bali ni vema kujua kuwa jina lenye laana hulaani na lenye baraka hubariki. Tunakutakia yaliyo mema na kama jina lako lilivyo basi uendelee kubarikiwa na kuneemeka. Hizi ni sala za wazazi wako.

Oikale nemilembe