Saturday, November 22, 2008

Katika Jina la Demokrasia.

Salamu za marejeo toka kwake Msangi Mdogo

Wapendwa katika jina la Watanzania. Amani iwe juu yenu. natumai wote muwazima.
Hii ni kuwataarifu rasmi kuwa, baada ya kimya cha muda mrefu sana, mahangaiko ya hapa na pale na mambo mengine, hatimaye ndugu, kijana, mpiganaji, muungwana na mpigikaji mwenzenu nimerejea ulingoni. najua kuna ambao walikuwa wangali wakinisaka katika www.msangimdogo.blogspot.com....... na najua kuwa kuna wale ambao watakuwa huenda ni wapya kabisa katika taarifa hizi. Ila nyote kwa ujumla, napenda kuwataarifu rasmi kwa, maskani yangu kwa sasa ni www.uchambuzi.blogspot.com
Kuna kitabu cha wageni pale, makala zangu zilizotangulia ambazo zilitoka katika sehemu mbalimbali nilizozurura nakadhalika. Ila hatimaye, nimeamua kutulia hapo. nawakaribisheni sanjari na kuwaomba muwafikishie ujumbe huu "Blogaz" wenzenu ambao mnawafahamu, pamoja na kuniwekea taarifa hizi katika blogi zenu kwa wale watakaoweza.
Mwisho kabisa, naomba wale ambao viungo vyao (link za blogi zao), haziko katika blogi yangu, wanitumie kwa mail ili niweze kuviweka pale, maana nataka kila mtu niwe na anwani ya kuingia kwenye maskani yake kwa urahisi. na kwa wale ambao wana nembo, pia wanaweza kunitumia ili zikae pale kama zilivyo za dada katabazi, Bongo Celebs nk.
Amani iwe juu yenu
Msangi, Ramadhani S.

Kaka. Ni katika jina jema lenye Amani, Heshima na Upendo twakukaribisha tena. Uwanja ni mwema, msafi na wenye uelimishaji. Blogs zaendelea kukwamua na kuonesha yale ambayo yanatakiwa na jamii na kwa namna hii tunaelekea ambako tutajivunia kuwa kweli sasa hizi ni Blog za jamii, kwa jamii. Na hii yastahili kuwa CHANGAMOTO YETU sote wenye kumiliki Blogs. Yaani kuwa sauti za wale wasioweza kujisemea.
  Tuko Pamoja Kaka

  

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

karibu sana

MARKUS MPANGALA said...

kaka kawaida yangu ni kufungua mashtaka kwa wale wote wanaoanzisha blogu halafu wanapotea. Lakini nimeghairi kwa bwana Rama Msangi naona karudi kama ule wimbo wa Squiza 'NAJA' kwa makeke na vurugu mpka wazungu na mablack waselebuka tu. Mkuu karibu tena nyumbani na karibu tena nyasa