Tuesday, November 18, 2008

Natamani kuwa mwalimu. Shule iwe UN na wanafunzi ma-Raisi

Ingenichukua muda kusahihisha Homeworks, lakini wote wangefanya VEMA dunia ingekuwa sehemu bora ya kuishi kuliko ilivyo sasa.

Napenda old style ya ualimu ambapo walimu walikuwa wanajua uwezo wa takribani kila mwanafunzi. Walikuwa wanahakikisha kuwa kila mtu anafanya "homework" yake na walikuwa wanasahihisha siku inayofuata. Walimu walikuwa na uwezo wa kutambua kama umefanya mwenyewe homework yako ama umefanyiwa. Halafu kingine nilichokuwa napenda ni ile style ya kubandika matokeo darasani. Yaani kujua nani kawa wa kwanza na nani wa mwisho. Hapo ilikuwa ni lazima usome sana maana ni kuangalia nani ana VEMA nyingi na nani anaongoza darasa. Lakini kwa mtazamo wangu ilikuwa na faida maana yaliyotendeka ilikuwa ni CHANGAMOTO KWETU kuongeza juhudi katika masomo.
Style hii ningeipata nikaweza kuitumia UN naamini ingesaidia saana. Yaani kuhakikisha kila maraisi wanapoondoka wanapewa "homework" ya kufanya nchini mwao na wakirejea kwa "darasa" (kikao) kijacho kwanza tunaangalia nani kafanya nini na kafanikiwa mangapi kisha tunasonga mbele. Yaani kujua nani anajua na kutatua matatizo ya nchini mwake na kuwasaidia wananchi wake na pia tungejua nani hana ajualo kuhusu shida na mahitaji ya wale awaongozao. Ingetuwezesha kujua nani yuko mstari wa mbele kubadilishana mawazo (pale nitakapowapa group discussion ya kukokotoa maswali) na kutumia "ideas" za wenzake kufanya homework zake kuwasaidia wananchi wake. NINA UHAKIKA kwa mfumo huu lazima ULIMWENGU ungekuwa hatua kadhaa mbele kuelekea kwenye mafanikio ya kutatua shida za wenye uhitaji.
Kwani wanapokutana huwa hawapewi majukumu ya kutekeleza? Ama wakipewa wanaweza kuyatekeleza bila kuwaeleza wananchi? Lakini kama ni majukumu kwa wananchi si tungeona mabadiliko huko tuliko? Namaanisha hata kama hatuambiwi si tungejua kuwa "ujenzi wa hizi zahanati ni manufaa ya raisi kwenda kwenye mkutano wa mwaka huu?" Najiuliza kama kuna mwananchi anayeweza kujibu akiulizwa amenufaika nini na raisi wake kwenda kwenye vikao vya Umoja wa Mataifa na vingi" Sisemi hatujanufaika, ila kama manufaa hatuyaoni bayana na hatuambiwi pia, sijui tufikirieje matumizi ya kodi zetu!

Anyway, japo kuna ukweli ndani yake, lakini nafikiri hii ni njozi. Never Mind!!!

3 comments:

Unknown said...

Habari za asubuhi mzee wa changamoto.
Wakati najibu maoni yako uliyoweka kataika blog yangu jana usiku sikuweza kupitia katika blog yako ili kuona changamoto zako.
nakushukuru sana kwa michamgo yako.
Nikipata muda zaidi nitakutembelea kwenye blog yako na kuweka mawili matatu.
Nakutakia ualimu mwema.

Simon Kitururu said...

Umoja wa Mataifa ni wazo zuri !Tatizo hakuna umoja kwenye umoja huu. Halafu hata wote mkikubaliana Nchi moja yenye veto isipokubali hakuna kinachoendelea.:-(

Mzee wa Changamoto said...

Thx alot Kaluse, Simon. It's always great to be with y'all.
Blessings