Saturday, November 15, 2008

Ni Maandamano yasioenda ama maonesho ya maombi?

Picha zote toka kwa Kaka Bernard Rwebangira wa www.bongopicha.blogspot.com
"Assert your right to make a few mistakes. If people can't accept your imperfections, that's their fault" Dr David M.Burns
" I am careful not to confuse excellence with perfection. Excellence i can reach for; but perfection is GOD's business" Michael J Fox
Naamini jina la Blog (The way you see the problem is the problem) na nukuu za hapo juu zitaongoza mtazamo wa hili nionalo mimi.
Nimelelewa katika mazingira na familia iliyothamini dini na imani na hakuna dini isiyohimiza maombi. Hivyo nami nimekua nikitambua na kufanya maombi, na sio tu kwa namna waonavyo wazazi na ama walezi, bali kwa mujibu wa kitabu Kitakatifu tuaminicho. Ni kitabu hicho hicho kinachozungumzia juu ya KUFUNGA NA KUOMBA pamoja na KUOMBA KWA ROHO NA KWELI.
Na ni katika haya ninapopata shaka na namna baadhi ya sehemu za maombi zinavyoendesha shughuli zao. Kufunga na kuomba halisi (ninavyofahamu mimi) ni kule ambako unakufanya ilhali humfanyi mtu mwingine asiyejua kinachoendelea katika "programu" yako ya siku kuona udhaifu wa mwili ama sura. Yaani asiyehusika asitambue mfungo kwa unyonge ama udhaifu wa mwili wako. Ni kufanya mfungo na maombi bila kuwa kikwazo ama shaka kwa wengine. Na Kuomba kwa roho na kweli ni kule ambako unakuwa sehemu ambayo umetoa muda, mwili na mawazo yako kwa ajili hiyo. Ni sehemu ambayo haikufanyi ufikirie kingine zaidi ya "muungano" wako na MUNGU.
Sasa nikirejea kwenye mkusanyiko kama huu ambao Jumapili iliyopita ulikutana kwa nia njema ya kuiombea serikali kufanya maamuzi bora nabaki na maswali kadhaa.
1: Hivi ni kweli kwamba waumini walikuwa wengi kiasi cha kuhitaji sehemu kama Mnazi Moja? Ama ni kutaka kuweka nguvu za pamoja katika maombi? Lakini si kama wana "sharika" wangeomba huko waliko na kusikika? Naamini kuwa MAOMBI YANA NGUVU NA MWENDO KASI kuliko tunavyoweza kufikiri.
2: Kama Waislamu nao wataendesha yao Ijumaa, kisha Hindu nao wakawa na yao kuunga mkono ama kupinga, kisha Wayahudi wakafanya, Bahai nao wakasaka siku yao, na wengine wenye imani tofauti wakaamua kufanya maombi yao, tutabaki tukiona hayo kama maombi ama majibishano? Na kama kuna uwezekano huo kwanini yaanzishwe?
3: Hivi kunakuwepo kuomba kwa roho na kweli wakati unajua kuna Kamera za picha na video, Kelele za magari na wapiga debe, dhihaka na pilika za siku zikiendelea? Kweli watu wata-concentrate kwenye maombi ya dhati bila kuogopa kuwekwa kwenye kumbukumbu ama wengine wataacha kuigiza kuwa katika maombi halisi ili wawekwe kwenye hizo kumbukumbu zitakazowaonesha kwenye magazeti, mitandao na televisheni mbalimbali?
Sina hakika na mtazamo wa wengine na sidhani kama ni lazima niendane na mtazamo wao maana kama hili ni tatizo basi kila mtu analiona toka katika upande wake na namna tuonavyo ndilo tatizo, na kama huoni tatizo katika hili, basi utaona tatizo kwa mimi kuliona tatizo na hilo litakuwa tatizo, maana namna uonavyo tatizo ndilo tatizo.
Kwangu sijaona umuhimu wa kufanya maombi ya kuiombea Serikali tena mahala kama Mnazi Mmoja. Naona tofauti ndogo saana ya hili na MAANDAMANO YASIYOENDA AMA KUTEMBEA na najitahidi kutoamini kilichopo kichwani kuwa kama hakukuwa na maombi halisi kulingana na mazingira, basi haya yaliyopangwa kuwa maombi kwa serikali yalikuwa MAONESHO YA MAOMBI
MUHIMU: Hapo juu ni mtazamo wangu na ushauri wangu ni kwamba, Ukiona tatizo soma jina la blog, ukidhani nimekosea soma nukuu ya kwanza na kama unadhani nafikiri niko sahihi angalia nukuu ya pili.
J'mosi njema



6 comments:

Christian Bwaya said...

Nimependa kichwa cha posti. Kumbe taizo si tatizo lenyewe, ni namna tunavyolichukulia! Kazi nzuri kaka. Naandika kukukaribisha kwenye ulimwengu huu wa kublogu.

Mzee wa Changamoto said...

Asante sana Kaka Bwaya. Nakushukuru kwa kunikaribisha nami kunitembelea pia.
Ni faraja kutembelewa na wakongwe kama nyie nami narejesha heshima kwako.
Blessings

Anonymous said...

Kweli mengine hayaaingii akilini.

Anonymous said...

Watu wanauhuru wa kumuomba Mungu popote ambapo wanaruhusiwa,ikiwa mioyo yao inamtazama Mungu wewe unashida gani waache waombe hata kama ni wapi,isiwe tu kutukana imani za wengine kwisha kazi pepo mkubwa weeeeeeeee

Anonymous said...

Unabania visu,huna maana huwezi kutukana wakati watu wanaombea taifa, wewe ni dini gani hata kama we ni rastafarian si tabia yao kutukana dini halafu unajifanya mkiristo wa huko uhayani.

Mzee wa Changamoto said...

Thx anon. Mmesoma aya ya mwisho? Kama mmesoma nadhani namna muonavyo tatizo ndilo tatizo.
Asante kwa "gut" za kutoa maoni.
Karibuni tena