Nimeikuta hii kwenye Blog ya Jamii nami nikaona ni vema kumuweka hapa jamvini ili wenye uhitaji wa nyimbo za injili waweze kumtembelea. Ni Prof Masangu Matondo Nzuzullima ambaye ameanzisha blog yake ya Nyimbo za Injili unayoweza kuitembelea kwa kubofya hapa
Sunday, December 21, 2008
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Mzee wa Changamoto;
"The Way You See The Problem Is The Problem". Japo nimesoma vitabu vingi sana vya falsafa nilikuwa bado sijakutana na msemo huu. Ni msemo unaokata katika kiini kabisa cha fikra na kutufanya tutafuta mtazamo mpya wa kufikiri. Kulingana na Euphrase Kezilahabi (mwandishi na mwanafalsa nimpendaye sana) tatizo kubwa lililopo katika jamii ni kwamba watu wamekoma kufikiri na kwa hivyo hakuna mawazo mapya na wachache waliyonayo hawasikilizwi. Matokeo yake ni kwamba jamii nzima imebakia kuimba kauli mbiu zile zile fishe ambazo hazikutufikisha popote na mawazo ya zamani yaliyoshindwa bado yanatawala. Ni kweli, tunahitaji kuyatazama matatizo yetu kwa mtazamo mpya na kuyatafutia masuluhisho mapya. Nimeguswa sana na kauli mbiu ya blogu yako. Pia asante sana kwa kuchukua muda wako kuliweka tangazo la blogu ya injili hapa. Noeli njema na Mwaka mpya (2009) wenye heri!!!
Post a Comment